
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi na Mfalme Abdullah II wa Jordan wamekutana mjini Cairo siku ya Jumatatu, Aprili 7, siku ya kwanza ya ziara ya rais wa Ufaransa nchini Misri. Lengo la mkutano huu wa pande tatu lilikuwa ni kuonyesha nia yao ya pamoja ya kutoa ushawishi ili kufikia kurejea kwa usitishaji vita huko Gaza na kuandaa suluhu la kisiasa.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu maalum huko Cairo, Valérie Gas
Viongozi hao watatu wa Misri, Jordan na Ufaransa wanatumai kuwa na ushawishi zaidi katika kuwasilisha ujumbe wa kipaumbele: ule wa “kurejeshwa mara moja kwa usitishaji vita” huko Gaza, ambapo wametoa wito kwa mara nyingine tena katika taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano wao, uliochukua takriban saa mbili Jumatatu, Aprili 7, na wakati ambapo wamejadili suala muhimu la utawala katika eneo hilo.
Emmanuel Macron aliweka wazi katika taarifa yake mapema siku hiyo: Hamas lazima isiwe na jukumu lolote katika kuitawala Gaza na isiwe tishio tena kwa Israeli. Mamlaka iliyoimarishwa ya Palestina inapaswa kuongoza ukanda wa Gaza kwa “uungaji mkono wa kikanda na kimataifa,” wamesema viongozi hao watatu, ambao wameahidi kuunga mkono juhudi zake.
Wasaidizi wa rais wa Ufaransa wanaeleza kwamba kwa hakika kuna suala la “uaminifu” kwa Mamlaka ya Palestina kwa wakazi wa Gaza, ambako Hamas ilikuwa madarakani, na kwamba mageuzi ni muhimu. Lengo ni kuishawishi Washington kuunga mkono mpango wa Waarabu wa kutoka katika mgogoro huo na kufungua upeo wa kisiasa.
Na kumkunja samaki wakati akiwa bado mbichi, wito kati ya viongozi hao watatu na Donald Trump umeandaliwa katika mpango wa Emmanuel Macron, kujadili hali ya Gaza. Hii ni njia ya mkuu wa nchi wa Ufaransa kufanya kama mpatanishi na Marekani, ambayo pia ina funguo za siku zijazo katika mgogoro huu.