Gaza: Israeli yashambulia hospitali ya Khan Younis, afisa wa Hamas auawa

Shambulizi la anga la Israeli limepiga Hospitali ya Nasser huko Khan Younis, kusini mwa ardhi ya Palestina, Jumapili, Machi 23, na kumuua afisa wa Hamas, kulingana na jeshi la Israeli na Hamas. Hamas imesema katika taarifa kwamba shambulio hilo limemuua Ismail Barhoum, mjumbe wa ofisi yake ya kisiasa.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Ulinzi wa Israeli Israel Katz amethibitisha katika taarifa yake kwamba lengo la shambulio hilo ni Ismail Barhoum, ambaye alikuwa akitibiwa katika Hospitali ya Nasser “baada ya kujeruhiwa vibaya katika shambulio la anga dhidi ya nyumba yake huko Khan Younis siku ya Jumanne,” wakati jeshi la Israeli lilipoanzisha mashambulizi makali ya anga katika eneo hilo baada ya usitishwaji mapigano wa miezi miwili, chanzo cha Hamas kimeliambia shirika la habari la AFP.

Jeshi la Israeli, kwa upande wake, limesema limefanya “shambulio usahihi dhidi ya gaidi muhimu wa Hamas anayendesha shughuli zake ndani ya hospitali hiyo.” Vuguvugu la Waislam wa Palestina “linatumia miundombinu ya kiraia, na kuhatarisha watu wa Gaza,” jeshi la Israeli limesema.

Kulingana na Wizara ya Afya ya Hamas, shambulio hilo limesababisha vifo vya watu wawili, ikiwa ni pamoja na mvulana wa umri wa miaka 16 ambaye alikuwa amefanyiwa upasuaji siku ya Ijumaa, na majeruhi kadhaa “ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa matibabu ambao walijeruhiwa kwa viwango tofauti.” Shambulio hilo limelenga “jengo la upasuaji ndani ya Hospitali ya Nasser, ambayo huhifadhi wagonjwa wengi na majeruhi” na kwamba “moto mkubwa” ulizuka katika hospitali hiyo.

Mlipuko huo “umesababisha hofu, na kusababisha uhamisho kamili wa idara ya upasuaji, ambayo imeharibiwa kwa kiasi kikubwa,” Wiozara ay Afya ya Hamas imeongeza. Kulingana na picha za AFPTV, moto ulizuka kwenye eneo la nje kwenye ghorofa ya pili ya jengo lililoathiriwa.

Maafisa kadhaa wakuu wa Hamas waliuawa tangu Jumanne

Tangu Jumanne, maafisa kadhaa wakuu wa Hamas wameuawa katika mashambulizi ya Israeli. Hamas imethibitisha siku ya Jumapili kifo cha Salah al-Bardawil, mjumbe mkuu wa ofisi yake ya kisiasa huko Gaza, aliyeuawa katika shambulio la anga la Israeli siku iliyotangulia huko Khan Younis. Kiongozi wa serikali ya Gaza Essam al-Dalis na Yasser Harb, wanachama wengine wawili wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, waliuawa katika mashambulizi ya Jumanne kwenye mji wa kusini wa Gaza.

Hamas kisha ikatoa “taarifa ya rambirambi” ambayo pia iliorodhesha majina ya Jenerali Mahmoud Abu Watfa, mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, na Jenerali Bahjat Abu Sultan, mkurugenzi mkuu wa idara ya usalama wa ndani.

Hamas imedhoofishwa na kifo cha viongozi wake wengi

Hamas imedhoofishwa kwa kiasi kikubwa na vifo vya viongozi wake wengi, ndani na nje ya Ukanda wa Gaza, tangu kuanza kwa vita vilivyochochewa na mashambulizi yake ya umwagaji damu dhidi ya Israeli mnamo Oktoba 7, 2023. Lakini bado iko mbali na “kuangamizwa,” kinyume na lengo la vita lililowekwa na Benjamin Netanyahu.

Mkuu wa mrengo wa kisiasa wa Hamas, Ismail Haniyeh, aliuawa mjini Tehran Julai 31, 2024, katika mlipuko uliodaiwa na Israeli, na mrithi wake, Yahya Sinwar, alifariki Oktoba 16 huko Gaza, pia aliuawa na jeshi la Israeli. Nafasi yake ilichukuliwa na kaka yake, Mohammed.

Kulingana na vyanzo kadhaa ndani ya vuguvugu la Kiislamu, mlinzi wa Yahya Sinwar, Mohammed Hassan al-Amour, pia aliuawa wakati wa usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili katika shambulizi nyumbani kwake huko Khan Younis.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *