Gaza: IsraelI yakiri kulipa silaha kundi la Wapalestina wanaopingana na Hamas

Mamlaka ya Israeli imekiri kuunga mkono na kulipa silaha kundi la Wapalestina wanaoipinga Hamas katika Ukanda wa Gaza, wakidai kuwa hii inatimiza “malengo yao ya vita” na “kuokoa maisha ya wanajeshi” wanaohusika na mashambulizi dhidi ya vuguvugu hilo la Kiislamu katika ardhi ya Palestina.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Ndiyo,” Brigedia Jenerali Effie Defrin, msemaji wa jeshi la Israeli, amejibu katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa, Juni 6, alipoulizwa kama taasisi yake “inapendelea” kusambaza silaha kwa wanamgambo katika Ukanda wa Gaza. “Tunachukua hatua kwa njia mbalimbali dhidi ya serikali ya Hamas,” ambayo “kuanguka” ni mojawapo ya “malengo yake ya vita,” afisa huyo ameongeza. “Ili kufanikisha hili, tunatumia mbinu mbalimbali [lakini] siwezi kusema zaidi.”

Siku moja kabla, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alithibitisha taarifa za mjumbe wa bunge, Avigdor Lieberman, waziri wa zamani wa ulinzi, ambaye alifichua kwa shirika la utangazaji la umma la Israel Kan kwamba serikali “inatoa silaha kwa kundi la wahalifu na wakosaji.”

“Ni vizuri tu,” Benjamin Netanyahu amesema

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israelina Palestina, kundi hili linawaleta pamoja watu wa kabila la Bedui linaloongozwa na Yasser Abu Shabab. Baraza la Mahusiano ya Kigeni la Ulaya (ECFR) linamtaja Yasser Abu Shabab kama kiongozi wa “genge la wahalifu linaloendesha harakati zake katika eneo la Rafah [mji unaozunguka Ukanda wa Gaza na Misri] na anayeshutumiwa kwa kupora lori za misaada” huko Gaza.

“Lieberman alifichua nini? Kwamba vyanzo vya usalama vimeanzisha kundi la Wagaza ambao wanapinga Hamas? Kuna ubaya gani hapo?” Benjamin Netanyahumekatika video iliyorushwa kwenye akaunti yake ya X siku ya Alhamisi. “Hakuna Ni vizuri tu,” ameongeza. “Inaokoa maisha ya wanajeshi wa Israeli” katika Ukanda wa Gaza, ambako Israeli imekuwa ikipigana na Hamas tangu shambulio lake ambalo halijawahi kushuhudiwa katika ardhi ya Israeli mnamo mwezi Oktoba 7, 2023, ambalo lilizusha vita.

Kundi la Abu Shabaab limechagua “njia ya uhaini na wizi,” kulingana na Hamas

Kulingana na ECFR, Yasser Abu Shabaab “hapo awali alifungwa na Hamas kwa ulanguzi wa madawa ya kulevya. Kaka yake aliripotiwa kuuawa na Hamas wakati wa kukabiliana na mashambulizi ya kundi hilo dhidi ya misafara ya misaada ya Umoja wa Mataifa.” Ikijibu ufichuzi wa Israeli kuhusu ukoo wa Abu Shabaab, Hamas ilitangaza kwamba kundi hilo “limechagua njia ya uhaini na wizi” na kuwataka raia kuupinga.

Hamas, ambayo ilichukuwa mamlaka huko Gaza mwaka 2007, inadai kuwa na ushahidi wa “uratibu wa wazi kati ya makundi haya ya waporaji, washirika wa wavamizi [Israeli] na jeshi la adui lenyewe katika uporaji wa misaada na uzushi wa migogoro ya kibinadamu ambayo inazidisha mateso” kwa Wapalestina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *