Gaza: Israeli yadai kuwaua viongozi wa kundi linaloshirikiana na Hamas

Kundi la Kataeb Al-Mujahideen, kundi dogo linaloshirikiana na Hamas katika eneo la Palestina, limelengwa na jeshi la Israeli katika mji wa Gaza. 

Imechapishwa:

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wao, Assad Abu Sharia, na kiongozi mwingine, Mahmoud Kaheel, wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la anga la Israeli, kulingana na taarifa ya kijeshi. 

Kulingana na jeshi la Israeli, kundi hili lilikuwa likiendesha harakati zake haswa wakati wa shambulio la Oktoba 7, 2023, na wanahusika moja kwa moja na utekaji nyara wa Shiri Bibas na wanawe, Ariel na Kfir. Familia ya Bibas imetoa hisia zake mara moja: “Habari hizi kwetu ni hatua muhimu katika mchakato wa kuomboleza na kukubali hasara hizi kubwa,” mwakilishi wa familia amesema katika taarifa. Maafisa wa kijeshi pia wanadai kuwa miili ya mateka watatu waliorejeshwa makwao katika siku za hivi karibuni pia ilitekwa nyara na kuuawa na kundi hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *