
Vuguvugu la Kiislamu la Palestina la Hamas limetangaza Jumapili, Mei 11, nia yake ya kumwachilia mateka wa Israeli ambaye ana uraia wa Marekani Edan Alexander katika tarehe ambayo haijatajwa, baada ya kuripoti mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani huko Doha. Donald Trump ameita tangazo hilo “habari kuu.” Siku ya Jumatatu, Waziri Mkuu wa israeli Benjamin Netanyahu almesema kuwa kuachiliwa huru kwa mateka huyo hakutasababisha kusitishwa kwa mapigano au kuachiliwa kwa wafungwa wa Kipalestina.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Tangazo la Hamas la kuachiliwa kwa Edan Alexander kutoka Gaza linakuja kabla ya ziara ya Rais wa Marekani Donald Trump katika Mashariki ya Kati, ambayo itampeleka Saudi Arabia, Qatar, na Falme za Kiarabu kuanzia Mei 13 hadi 16. Katika mtandao wake wa Truth Social, amekaibisha tangazo hili la Hamas kama “habari kuu,” akisema anatumai kuwa kuachiliwa kwake itakuwa “hatua ya kwanza kwa hatua za muhimu za mwisho za kumaliza mzozokati ya Israeli na Hamas unaodumu zaidi ya mwaka mmoja na nusu.”
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema siku ya Jumatatu, Mei 12, kwamba kuachiliwa kwa Edan Alexander hakutapelekea kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza au kuachiliwa kwa wafungwa wa Kipalestina. Katika taarifa kutoka ofisi yake, Benjamin Netanyahu, kinyume chake, amesisitiza kwamba mazungumzo ya uwezekano wa makubaliano ya kuachiliwa kwa mateka wote huko Gaza yatafanyika “chini ya mashalbulizi” na kwamba nchi yake inajianda “kuzidisha mapigano.”
Hii inakuja wakati familia ya Edan Alexander ilisema katika taarifa kwamba wanatarajia kuachiliwa kwake “katika siku zijazo.”
Edan Alexander, mateka pekee aliye hai ambaye ana uraia wa Marekani bado anashikiliwa huko Gaza, alitekwa nyara wakati akihudumu na kitengo cha wasomi kusini mwa Israeli wakati wa shambulio ambalo halijawahi kufanywa na Hamas mnamo Oktoba 7, 2023. Shambulio hilo lilizusha vita huko Gaza, ambapo Israeli, ikiapa kuiangamiza Hamas, iliaanzisha mashambulizi makubwa ya kulipiza kisasi na kusababisha vifo vya watu elfu kumi.
Kutokuwa na uhakika juu ya tarehe ya kuachiliwa kwa mateka
Mateka Edan Alexander anatarajiwa kuachiliwa ifikapo kesho, Jumanne, ikiwezekana saa sita mchana leo, kulingana na vyanzo vingine. Mabadiliko ya kushangaza ya matukio ambayo yanakuja wakati mazungumzo kati ya Israeli na Hamas yamesimama, anaripoti mwandishi wetu huko Jerusalem, Michel Paul. Jukwaa la familia za mateka linatumai kuwa kuachiliwa huku kutaleta makubaliano mapana zaidi ya kuruhusu kurejea kwa mateka wote ambao bado wanashikiliwa huko Gaza.
“Edan Alexander ataachiliwa kama sehemu ya juhudi za kufikia usitishaji vita, kufungua vivuko na kuruhusu misaada na kuingia kwa watu wetu huko Gaza,” Hamas imesema katika taarifa. Hamas imesema iko “tayari kuanza mara moja mazungumzo ya kina kwa nia ya kufikia makubaliano ya uhakika juu ya kumaliza vita, kubadilishana (mateka wa Israel kwa wafungwa wa Kipalestina), usimamizi wa Gaza na chombo huru (…) pamoja na ujenzi mpya na mwisho wa kuzingirwa.”