
“Watu ulimwenguni kupitia televishei zao wanatazama mauaji ya halaiki moja kwa moja huko Gaza kwenye ,” Amnesty International inalaani. Kila siku, picha za kutisha zinaibuka kutoka kwa eneo hili la Palestina, lililodumazwa na mabomu ya Israeli.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Jerusalem, Sami Boukhelifa
Mauaji hayo yalirekodiwa na Wagaza wenyewe. Huku idadi ya vifo ikizidi 52,000, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu anaanza “kufikiria kumaliza vita” ndani ya miezi michache, kulingana na vyombo vya habari vya Israeli.
“Mapigano yangeisha ifikapo Oktoba 2025, baada ya takriban miaka miwili ya vita,” kulingana na Gazeti la Israeli la HaYom, likinukuu vyanzo vya karibu vya Benjamin Netanyahu. Hadi sasa, Waziri Mkuu wa Israeli amekuwa akikataa kutaja mwisho wa mashambulizi ya mabomu na uvamizi wa wanajeshi wake huko Gaza. Kurudia tena na tena kwamba vita vingekuwa “refu na ngumu.” Kauli hizi zinakuja wakati ambapo Washington inaelezea nia yake ya kukomesha hali hii.
Lakini mwisho wa vita haimaanishi mwisho wa uvamizi wa kijeshi. Katika hotuba yake mapema wiki hii, Benjamin Netanyahu alionya: “Hamas haina nafasi huko Gaza. Na vile vile Mamlaka ya Palestina. Kwa nini muondoe utawala unaotaka uharibifu wetu na kuweka utawala mwingine unaotaka uharibifu wetu?” Israel inakataa suluhisho lolote la kisiasa.
Wakati huo huo, huko Gaza, raia wanakumbwa na mauaji ya kila siku. Na Waziri Mkuu wa Israel anaendelea kutetea kuondoka kwa “hiari” kwa Wagaza. Jaribio la utakaso wa kikabila chini ya sheria ya kimataifa.