Gavana wa kijeshi wa Kivu Kaskazini DRC auawa katika mapambano na kundi la M23

Gavana wa kijeshi katika Jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC amefariki dunia kutokana na majeraha aliyopata wakati wa mapambano kati ya jeshi la serikali na waasi wa M23 huko Goma, makao makuu ya jimbo hilo.