Gabon: Rais mteule Brice Oligui Nguema akabiliwa na changamoto nyingi

Nchini Gabon, Brice Clotaire Oligui Nguema, aliyechaguliwa kwa alama ya “mtindo wa Kisovieti” ya 90.35% ya kura, na ushiriki wa 70.4%, kulingana na takwimu za muda kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, sasa anasubiri tu uthibitishaji wa mahakama ya kikatiba kuendelea kusalia madarakani kwa miaka 7 kama rais wa jamhuri, wadhifa ambao ameshikilia kwa miezi 20. 

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum huko Libreville, François Mazet

Baada ya kipindi hiki cha mpito ambacho hakuna kitu kilionekana kumtia doa mbaya kama mshindi wa familia ya Bongo, itabidi akabiliane na changamoto nyingi na muhimu.

Nchini Gabon, ambako kuna matumaini makubwa, pia kuna uwezekano mwingi wa kukatishwa tamaa. Brice Clotaire Oligui Nguema anaonekana kuelewa hili. Mapema jana asubuhi, wakaazi wengi wa Libreville walipotatizika kufika kazini baada ya kusherehekea kuchaguliwa kwake, alitoa onyo hadharani kwa timu ya rais mara tu baada ya sherehe ya kupandisha bendera. “Watu wa Gabon wanatarajia mengi kutoka kwetu,” alitangaza. “Asilimia 90.35 ni uthibitisho wa dhiki inayowakabili. Uchaguzi ulikuwa jana, hatuishii kwa ushindi, ushindi ni kazi inayoendelea.”

Alieleza kuwa bado anawahitaji “maafisa wazamani” huku wengi wakimkosoa kwa kuendelea kuwa karibu naye kikosi cha walinzi wa zamani katika enzi za Bongo. Anategemea uzoefu wao ili kukabiliana na changamoto zilizopo. Changamoto za kisiasa tayari, pamoja na muungano mpana sana unaomzunguka ambao utahitaji kudhibitiwa, lakini pia changamoto za kijamii, na mahitaji makubwa kuhusiana na mahitaji ya kila siku, kama vile upatikanaji wa maji, umeme, barabara au ukarabati wa shule. Haswa, changamoto za kiuchumi: mpito umeanzisha sera kabambe ya bajeti ya matumizi, lakini ambayo ni ngumu kufadhili, haswa ikiwa bei ya mafuta itabaki chini sana.

Mashtaka ya udanganyifu  yatupiliwa mbali

Wafuasi wa kiongozi wa mpito wanafutilia mbali tuhuma zozote za udanganyifu na matumizi makubwa ya rasilimali za serikali. Mgombea aliyeshindwa Alain-Claude Billie-By-Nze anabaini kwamba uchaguzi huu ulikumbwa na udanganyifu ulishuhudiwa katika utawala wa zamani. Lakini hatapinga matokeo. Shutuma za udanganyifu, hata hivyo, zimefutiliwa mbali na Anges-Kevin Nzigou, mratibu wa Mkusanyiko wa Wajenzi.

Anges-Kevin Nzigou, ambaye alitangaza mnamo Aprili 14 mabadiliko yajayo ya Mkutano wa Wajenzi wa Majukwaa kuwa chama cha kisiasa kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi ujao wa wabunge, kwa lengo la kuwa kitovu cha wengi wanaoweza kumtumikia Mkuu wa Nchi. Mkutano mkuu umeitishwa siku ya Jumamosi Aprili 19.

Hata hivyo, ujumbe wa waangalizi wa kimataifa ulikaribisha upigaji kura. Wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, ujumbe wa Umoja wa Afrika, ECCAS, Francophonie na Jumuiya ya Madola waliwapongeza raia wa Gabon kwa “ukomavu” wao. Jumuiya ya Madola, hata hivyo, ilionyesha ukosefu wa usawa wa upatikanaji wa nafasi ya vyombo vya habari kati ya wagombea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *