
Mshindi wa uchaguzi wa urais mnamo Aprili 12 kwa ushindi wa kishindo, Brice Clotaire Oligui Nguema ameapishwa katika uwanja wa michezo wa Angondjé, viungani mwa Libreville, Jumamosi, Mei 3, mbele ya viongozi wa Afrika wapatao kumi na tano waliokuja kwa hafla hiyo. Akiahidi kufanya kazi kuelekea “Gabon mpya”, hivyo akawa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tano ya Gabon, miezi 20 baada ya kupinduliwa kwa Ali Bongo.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Akiwa amewasili katika uwanja wa michezo wa Angondjé kwa gari lililokuwa wazi kabisa, Brice Clotaire Oligui Nguema pengine hakuhitaji kukatwa kwa umeme, hali iliyoioikumba Libreville wakati wa hafla ya kuapishwa kwake alasiri ya Jumamosi, Mei 3, ili kuwakumbusha watu kwamba ujenzi upya wa miundombinu ya Gabon ulikuwa mojawapo ya vipaumbele vya mamlaka yake mpya. Miongoni mwa vipaumbele hivyo, pia alitaja, katika hotuba yake ya kwanza kuwa rais kamili, mseto wa uchumi, vita dhidi ya ukosefu wa ajira kwa vijana, mabadiliko ya ndani ya maliasili na mapambano dhidi ya baadhi ya majanga, akianza na “kutokujali, rushwa, uchoyo, uvivu na uzembe.”
Njia ya raha itakuwa ndefu, lakini kwa kazi, nidhamu, bidii […] tutasonga mbelea na kufkia hatua kubwa.
Brice Clotaire Oligui Nguema aliapa, dakika chache mapema, mbele ya Mahakama ya Katiba, “kuheshimu na kutetea kwa uaminifu Katiba na utawala wa sheria”, kabla ya kutunukiwa kola ya urais ya Mwalimu Mkuu wa Daraja za Kitaifa na kupokea sifa za kitamaduni za mamlaka, ikiwa ni pamoja na tochi inayoashiria “mwanga, tumaini na uwajibikaji sirikishi” ambayo alimkabidhi Mamady Doumbouya katika pendekezo la ishara kwa rais wa mpito wa Guinea kumtaka pia kuandaa uchaguzi katika nchi yake.
“Asitusaliti kwa kuwa dikteta”
Hatimaye Brice Clotaire Oligui Nguema alichukua fursa ya hafla hiyo iliyomalizika kwa gwaride la kijeshi na wanajeshi kuruka kwa miamvuli, kuelezea kwa kina ratiba ya kuanzishwa kwa taasisi mpya za nchi: uchaguzi wa wabunge na serikali za mitaa utafanyika Septemba 27 na Oktoba 11, kabla ya uchaguzi wa maseneta kufanyika. Kuhusu mpito wenyewe, utakamilika Desemba 23, kwa kuapishwa kwa majaji wa Mahakaam mpya ya Katiba.
Katika uwanja wa michezo wa Angondjé, wakuu 16 wa nchi za Afrika walisafiri kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa Gabon, akiwemo Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, ambaye alipokea pongezi nyingi. Karibu nao pia: karibu watu 40,000 wenye shauku, kama mfuasi huyu wa Brice Oligui Nguema ambaye alisema sherehe hii “itasalia katika kumbukumbu za historia ya Gabon” huku mwingine akisifu “sherehe nzuri zaidi ya kuapishwa ambayo [amewahi] kuona, sherehe iliyojaa hisia na iliyojaa furaha ya pamoja kati ya rais na raia wake.” “Ilikuwa nzuri sana!” ” anahitimisha.
Ukweli unabaki kuwa katika bunge hili ambalo linamuunga mkono kabisa mkuu mpya wa nchi, wengi pia wanatarajia mengi kutoka kwake: “Asitusaliti kwa kuwa dikteta. “Lazima aendelee kufanya alichoanzisha: ndivyo tunavyotarajia kutoka kwake,” alijibu raia wa tatu kwa mwandishi wetu huko Libreville, Yves Laurent Goma.