Kiongozi wa kijeshi nchinik Gabon, Brice Oligui Nguema, amepata ushindi mkubwa kufuatia uchaguzi mkuu wa rais uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita, matokeo ya awali yakionesha amepata asilimia 90.35 ya kura zote.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Nguema, ambaye alimaliza utawala wa zaidi ya miongo mitano wa utawala wa familia ya Bongo mwezi Agosti mwaka 2023 aliahidi kurejesha utawala wa kiraia.
Awali, Wizara ya mambo ya ndani ilikuwa imetangaza kuwa, mwanajeshi huyo alikuwa amefaulu kupata kura zaidi ya laki 5 ambazo zilikuwa sawa na asilimia 90.3.
Aidha wizara hiyo ilithibitisha kuwa asilimia 70.4 ya wapiga walishiriki ambapo watu Milioni 2.3 walikuwa wameandikishwa.
Mpizani wake mkuu Alain-Claude Bilie By Nze, aliyehudumu kama waziri mkuu wakati wa utawala wa Ali Bongo, alipata asilimia tatu ya kura zote wakati wagombea wengine sita wakishindwa kufikisha zaidi ya asilimia moja.
Oligui Nguema kwa sasa anatarajiwa kuapishwa ambapo ataongoza taifa hilo kwa kipindi cha miaka saba, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa njia ya simu alimpongeza kwa ushindi wake.