Gabon: Jenerali Brice Oligui Nguema arasimisha nia yake ya kuwania urais

Rais wa mpito wa Gabon Jenerali Brice Clotaire Oligui Nguema almetangaza kugombea uchaguzi wa urais wa Aprili 12, 2025. Anajionyesha kama “mjenzi” ambaye, baada ya kuikomboa Gabon kulingana na kauli yake, anaahidi kujenga nchi yenye ustawi.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Brice Oligui Nguema ambaye ni rais wa mpito nchini Gabon tangu kuanguka kwa Ali Bongo katika majira ya joto ya mwaka 2023, ametangaza nia yake ya kuwania katika uchaguzi wa rais, duru ya kwanza ambayo imepangwa kufanyika Aprili 12.

Ilikuwa katika eneo kubwa la ujenzi wa kongamano la kimataifa ambapo Brice Clotaire Oligui Nguema alitangaza nia yake hiyo kugombea urais. Akijawa na shauku, mgombea huyo urais ameuambia umati: “Kwa upande wangu, niko tayari!” Tayari kuongoza hatima ya nchi yetu! »

Niko tayari kuongoza hatima ya nchi yetu.

Wakitoka kila pembe ya mji mkuu, wafuasi wa rais wa mpito walishangilia kwa furaha uamuzi huo. Mtu aliyepindua utawala wa Bongo amesikia wito wa kugombea. “Baada ya kutafakari kwa kina, na kujibu wito zenu nyingi, nimeamua kuwa mgombea,” amesema na huku umati wa wafuasi wake ukipokea kauli hiyo kwa vifijo na nderemo. “Oligui rais, Oligui rais! “, waliimba wafuasi wake, anaripoti mwandishi wetu Yves-Laurent Goma.

Wapinzani wake wanamtuhumu kwa kuongeza deni na kufungua maeneo mengi ya ujenzi, ambayo baadhi yake sasa yamesitiswa. “Mimi ndiye ninayewalipa madeni waliyotuachia,” jenerali amejibu. Amonyesha mafanikio yake makuu, miezi 18 baada ya mapinduzi yake: “Nimetengeneza kilomita 1,969 za barabara. Nimesambaza teksi 417 na 400 zaidi zitawasilishwa katika siku chache zijazo, na kutengeneza nafasi za kazi 817.”

Hapa anapotosha kwa sababu ana uwezo unaotolewa na Serikali., amesema Jean-Rémy Yama, mgombea urais, akijibu kuhusu kugombea kwa Brice Oligui Nguema

“Kila kitu kilipangwa tangu mwanzo ili kumruhusu kuwa mgombea na hasa kuhakikisha ushindi wake, ni hatua ambayo itauzwa na ambayo yeye ndiye mwamuzi na mchezaji”, aanasema Jean-Rémy Yama, mgombea urais, ambaye anahakikisha kwamba hatakubali kushindwa na bado ana matumaini “kwamba Wagabon watashangaza wengi” Aprili 12.

Masharti mengi ya kuwa mgombea

Kufikia Septemba 2, 2023, tarehe ya kutiwa saini kwa katiba ya mpito na siku nne baada ya “mapinduzi ya ukombozi” – kulingana na usemi uliotumiwa na jeshi lililomwangusha Ali Bongo Ondimba – wachambuzi wa kisiasa walibaini kuwa Brice Oligui Nguema, rais wa kipindi cha mpito, ndiye pekee aliyeidhinishwa kuwa na uwezo wa kugombea wadhifa wa juu. Kwa watendaji wengine wa mpito, imeonyeshwa kwenye mkataba: “Hawastahiki kugombea katika uchaguzi wa urais.”

Mkataba wa mpito pia unafafanua kundi la umri la kuwa mgombea wa mkuu wa Gabon: kati ya umri wa miaka 35 na 70, umri uliojumuishwa katika Ibara ya 43 yaa sheria ya msingi. Sheria ambayo inamtengaPierre Claver Maganga Moussavou. Masharti mengine ambayo yanaweza kupunguza idadi ya wagombea katika uchaguzi wa rais: wale wanaohusishwa na uraia.

Mwishoni mwa mwezi wa  Januari, Brice Oligui Nguema aliona kikwazo cha mwisho kinachomzuia kugombea kikifunguliwa. Ingawa wanajeshi walikuwa wameahidi kurudisha mamlaka kwa raia, kanuni za uchaguzi zilizopigiwa kura na Bunge zinawaruhusu kugombea urais ikiwa watajiuzulu au kuchukua likizo kutoka kwa jeshi.