
FOUNTAIN Gate Princess iliyopo nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu imesema kwa iliko sasa, inahitaji kushinda mechi tano tu ili kujihakikishia kuwa katika nafasi nne za juu.
Kocha mkuu wa timu hiyo, Mirambo Camil alisema hawakuanza vyema ligi kuu jambo na changamoto kubwa ni nje ya uwanja ikiwmao kukamilisha vibali vya wachezaji wa kigeni.
“Fountain ni miongoni mwa timu zenye ushindani kwa takribani miaka mitatu sasa, hatuangalii changamoto tena, mipango yetu sasa ni namna gani tunaweza kurudi kwa nguvu na kupambana angalau tumalize nafasi ya nne kwenye msimamo,” alisema Mirambo na kuongeza;
“Sisi tumecheza mechi 10, zimesalia nane kumaliza msimu, angalau tukipata pointi tatu katika mechi tano hizo tutakuwa tumefikisha 25 zilizosalia hata sare itatusaidia kwa kiasi kikubwa.”
Mbali na ratiba ya ligi kuu, Fountain itashiriki michuano ya Samia Women Super Cup ikianza na Yanga Princess kwenye nusu fainali itakayopigwa Machi 04.