
Rais wa zamani wa shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blatter na aliyekuwa rais wa shirikisho la soka la Ulaya, UEFA, Michel Platini, wameondolewa mashtaka na mahakama ya Uswis kufuatia rufaa waliyokata katika kesi ya rushwa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Kama ilivyokuwa awali, wakati wawili hawa walipoondolewa mashtaka mengine mwaka 2022, mahakama ya rufaa kwenye mji wa Mutttenz ulio jirani na Basel, haikufuata mapendekezo ya waendesha mashtaka waliotaka wapewe adhabu ya kifungo cha nje cha miezi 20.
Baada ya miaka 10 ya kesi, rufaa ya mwisho bado inawezekana kufunguliwa katika mahakama ya juu ya Uswis, lakini kwa kuzingatia vifungu kadhaa vya kisheria.
Blatter mwenye umri wa miaka 89 na Platini mwenye miaka 69, walikuwepo mahakamani katika kesi iliyohusu ucheleweshwaji wa malipo ya faranga za Uswis milioni 2 (Euro milioni 1.8) yaliyofanywa kwa akaunti ya Platini mwaka 2011 kama malipo ya ushauri wa kikazi.
Kesi hii ilizima ndoto za Blatter na nahodha wa zamani wa Ufaransa na baadae kocha Michel Platini, ambapo walikuwa miongoni mwa viongozi wa soka wenye nguvu na ushawishi mkubwa duniani.
Baada ya kuondolewa mashtaka mara mbili, waendesha mashtaka wanapaswa kukubaliana na ukweli kuwa wameshindwa kuendesha kesi hii. Michel Platini ni lazima sasa aache kufuatiliwa na kesi za jinai,” alisema Dominic Nellen, wakili wa Platini.
Kesi hii ilianza mwaka 2015 wakati Blatter alipoamua kuachia ngazi kama rais wa FIFA kufuatia kashfa za rushwa.
Wawili hawa walisafishwa na mahakama ya Uswis kwa mara ya kwanza mwezi Juni mwaka 2022 kwa makosa yote yaliyokuwa yanawakabili ikiwemo malipo ya ulaghai, kuvunja uaminifu na udanganyifu. Hata hivyo waendesha mashtaka wa Uswis walikata rufaa muda huohuo.
Upande wa utetezi na waendesha mashtaka wanakubaliana kuwa ni kweli Platini alimshauri Blatter katik ya mwaka 1998 na 2002 na kwamba mwaka 1999 wawili hao walitiliana saini mkataba kukubaliana malipo yam waka ya faranga za Uswis 300,000 zilizopaswa kulipwa na FIFA kwa ukamilifu.
Blatter na Platini wanasema mwanzoni walikubaliana kwa mdomo na bila ya mashahidi wowote kuhsuu mshahara wa shilingi milioni moja faranga za Uswis, lakini kanuni za kifedha za FIFA hazikuruhusu malipo hayo kufanywa mara moja.
Mwezi Januari mwaka 2011, ikiwa ni zaidi ya miaka 8 baada ya kumaliza mkatabawake kama mshauri wa Blatter, Platini anadai alianza kudai deni lake la faranga milioni mbili za Uswis, ambazo FIFA ililipa, wakati huo Blatter alikuwa akigombea kwa muhula mwingine kuwa rais wa FUFA na Platini alikuwa ameshinda kitu cha urais wa UEFA.
Waendesha mashtaka wanadai kuwa malipo haya hayakustahili, yalifanywa kinyume cha utartibu kwa kupindisha kanuni za FIFA kupitia nyaraka za kughushi kulikofanywa na viongozi wote wawili.