
Muda mfupi ujao Simba na Azam FC zitaumana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu baina ya timu hizo.
Mchezo wa mzunguko wa kwanza baina yao uliochezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, Septemba 26, 2025, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Hata hivyo utamu wa mechi ya leo unanogeshwa zaidi na makocha Fadlu Davids wa Simba na Rachid Taoussi wa Azam FC ambao chini yao timu hizo zimekuwa na matokeo mazuri kwenye Ligi msimu huu.
Fadlu ambaye alianza na Simba msimu huu, ameiongoza timu hiyo katika mechi 19 akishinda 16, kutoka sare mbili na kupoteza mchezo mmoja.
Katika mechi hizo 19, Simba imefunga mabao 41 na imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara sita huku ikiwa na asilimia 89.5 za ushindi.
Kwa upande wa Taoussi ameiongoza Azam FC katika michezo 19, imepata ushindi mara 13, imetoka sare tatu na kupoteza tatu.
Chini ya Taoussi, Azam imekuwa na asilimia 68.4 za ushindi na imefunga mabao tisa na kufungwa mabao 29.
Mchezo huo wa Simba na Azam FC utachezwa leo Februari 24, 2025 kuanzia saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.