Fadlu asema atamaliza mchezo ugenini, Steve hajaridhika na matokeo

Kocha Mkuu wa kikosi cha Simba, Fadlu Devid amesema kutokana na ukubwa wa timu hiyo haikutakiwa kupata matokeo ya bao 1-0 yameonesha kuwavunja moyo mashabiki wa timu hiyo.

Kocha Fadlu, amesema timu hiyo ilipaswa kushinda kuanzia goli mbili hadi nne wakati wakiwa uwanja wa nyumbani kwani wachezaji walishauzoea uwanja na hali ya hewa.

Fadlu ameendelea kuwatuliza mashabiki wa timu ya Simba, kuwa watulivu kwani bado wanayo nafasi ambayo wataitumia vizuri ili kufika fainali hilo ndio lengo la timu hiyo.

FD 01

Amesema watajipanga vizuri ili kuhakikisha wanaumaliza mchezo huo wakiwa ugenini, ingawaje utakuwa mgumu kwa upande wao kwa sababu ya kutouzoea uwanja na hali ya hewa ya huko.

Pia, amesema katika mchezo huo walikuwa na nafasi nzuri ya kucheza na kupata ushindi mnono ila kwa bahati mbaya matokeo yaliyopatikana ni hayo na mashabiki waupokee.

“Katika uwanja huu wa nyumbani tulikuwa nafasi kubwa ya kumaliza mchezo huo, kwa sababu hatujui uwanja wa huko utakuwaje kwa kwa upande wetu, lakini tutafanya mabadiliko kwa kuongeza uwezo na kiwango bora kwa wachezaji,” amesema Fadlu. 

Ameeleza, hiyo ni nafasi ya kwanza kucheza mchezo wa nusu fainali wakiwa nyumbani hivyo haiwakatishi tamaa na kuwavunja moyo kutoendelea kujipanga kwa mchezo unaofuata kwani nafasi bado ipo.

FD 02

Amesema akili za mashabiki wa timu hiyo, tayari ilishajipanga kuimaliza mechi hiyo wakiwa katika uwanja wa nyumbani.

Kwa upande wa kocha wa Stellenbosch, Steve Barker amesema hajaridhika na uamuzi uliotolewa kwa upande wa wapinzani wao kwani goli  likikuwa ni offside na sio goli halali.

“Sijaridhishwa na uamuzi ulitolewa katika muafaka wa goli lile, kwani uamuzi huo haukuwa sahihi ila nitajipanga na  nitawashinda katika uwanja wa nyumbani na nitafika fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika (CAF),” amesema Kocha  Steve.

FD 03

Kocha amesisitiza hauridhishwa na uamuzi ulitolewa kwani goli lilikuwa la wazi kuwa la Offside kwani wachezaji waliugusa mpira huo.

Amesema, mechi hiyo itarejewa katika uwanja wa kwao na wanaamini kuwa watashinda wakiwa kwao kwa sasa wanaenda kujipanga ili kumaliza hilo.

Amesema kutokana na uchezaji wa timu ya Simba alioushuhudia katika mchezo huo wataenda kumalizana wakiwa kwao.

FD 04

Hali ya mashabiki na matumaini yao

Licha ya timu ya Simba kutoka na ushindi wa bao moja dhidi ya wapinzani wao Stellenbosch, ila mashabiki wa timu hiyo wameonekana kutoka uwanjani wakiwa na huzuni kwa kutopendezwa na matokeo hayo.

Wakitoa maoni ya mchezo huo mashabiki wamesema timu hiyo haikutakiwa kutoka na goli moja bali walitakiwa kumaliza mechi wakiwa uwanja wa nyumbani.

Thabit Kombo, mkazi wa Paje amesema tumefurahi kwa kwa sababu hatukufungwa tukiwa nyumbani ila timu hiyo ilipaswa kuimaliza mechi mapema.

FD 05

Amesema, Wachezaji wa timu hiyo walikuwa na nafasi nyingi za kufunga magoli ila cha kushangaza waliishia kupoteza nafasi muhimu ambazo zingewaweka katika nafasi nzuri.

“Tumeshinda ila hatujaridhika kutokana na ushindi huu ambao tumetoka nao kwani tulikuwa na nafasi nyingi na nzuri za kushinda ila sio mbaya tutajipanga vizuri,” amesema Thabit.

Naye, Halima Abdalla Mkazi wa Fuoni amesema hawawezi kuwalaumu sana wachezaji kwani nao ni binadamu na ukiwa uwanjani tofauti na ukiwa nje.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *