EuroMed Rights: Mpango wa Trump ni kuunga mkono mauaji ya Kimbari dhidi ya watu wa Palestina

Kundi la kutetea haki za binadamu Ulaya-Mashariki ya Kati limeelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya pendekezo la hivi karibuni la Donald Trump la kuwahamishia wakazi wa Gaza na kuwapeleka Misri na Jordan, likitoa wito wa kuwepo upinzani mkali wa kikanda na kimataifa dhidi ya wazo hilo.