Euro-Med: Israel inatumia drone kuwatia hofu watu wa Gaza, inawatisha kwa ‘Nakba ya 2, ya 3’

Shirika la kutetea haki za binadamu la Euro-Mediterranean Human Rights Monitor limeonya kuwa utawala wa Kizayunii wa Israel unatumia ndege zisizo na rubani kama silaha ya kisaikolojia kuwatia hofu na wahka Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, na hivyo kuzidisha mashinikizo kwa wakazi wa eneo hilo ili wakubali mpango wa Marekani na Israel unaowalazimisha kuhama makazi yao.