
Umoja wa ulaya unataka serikali nchini Kenya, kufanya kila juhudi kuhakikisha mageuzi ya mfumo mzima wa uchaguzi yanafanyika kabla ya uchaguzi wa mwaka 2027 kuhakikisha uwazi katika uchaguzi huo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kwa mjibu wa Ivan Štefanec, ambaye aliongoza ujumbe wa ufwatiliaji uchaguzi wa umoja wa umoja wa ulaya nchini Kenya, tayari Kenya imeanz akupinga hatua katika kufanyia marekebisho mfumo wake wa uchaguzi ikiwa juhudi za sasa za kuwateua makamishna wapya wa tume ya uchaguzi.
Tume hiyo pia inataka tume ya chaguzi nchini Kenya, pewa pesa za kutosha kuendesha shughuli zake, ikiwemo kununua mfumo ya kisisasa ya teknolojia.
Licha ya hayo Štefanec amesema wametambua kuna ukosefu wa maendeleo ya wazi katika utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Ujumbe wa Uangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya EU, ya mwaka 2022, Stefanec akisema idade kubwa ya wadau waliowasiliana nao walikubaliana juu ya umuhimu wa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) isioegemea upande wowote.
Uchaguzi wa mwaka 2022
Mwaka wa 2022, ujumbe wa waangalizi wa chaguzi wa umoja wa Ulaya ulitoa mapendekezo 21, yakiwemo mapendekezo saba yaliyopewa kipaumbele, kulingana na uchunguzi, na wadau mbalimbali.
Mapendekezo hayo yalijumuisha, miongoni mwa mengine, kutoa fedha za kutosha kwa IEBC kwa ajili ya elimu endelevu ya wapiga kura, kuboresha teknolojia ya uchaguzi kupitia ukaguzi wa mara kwa mara na mashauriano na wadau, kuwezesha utekelezaji wa Sheria ya Ufadhili wa Kampeni za Uchaguzi ili kudhibiti matumizi ya kampeni kwa ufanisi, kufafanua kisheria maana ya matamshi ya chuki kulingana na wajibu wa kimataifa wa haki za binadamu, kuondoa vifungu vya 22 na 23 vya Sheria ya Matumizi Mabaya ya tarakilishi na kuanzisha taratibu wazi za usimamizi wa wafanyakazi na taarifa katika vituo vya kuhesabu kura ili kuongeza imani miongoni mwa wapiga kura.
Taarifa ya AU imekuja kipindi aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Kenya, Wafula Chebukati akifariki usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa kipindi kirefu.