EU yasikitishwa na vikwazo dhidi ya majaji wanne wa ICC

Tume ya Ulaya imesisitiza kuiunga mkono kikamilifu mahakama hiyo yenye makao yake makuu mjini The Hague.

Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, ameandika kwenye ukurasa wake wa X akisema “ICC inawa-wajibisha wahusika wa uhalifu duniani na inawapa sauti waathiriwa, na hivyo ni lazima iwe na uhuru wa kuchukua hatua bila kushinikizwa.”

Msemaji wa Tume ya Umoja wa Ulaya, Anitta Hipper, amesema vikwazo hivyo kwa sehemu vinatokana na kutolewa kibali cha kukamatwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na kutokana na juhudi za Marekani za kuiondoa mahakama hiyo.

Majaji waliowekewa vikwazo ni Beti Hohler kutoka Slovenia, Reine Alapini-Gansou kutoka Benin, Luz del Carmen Ibanez Carranza raia wa Peru na Solomy Balungi Bossa kutoka Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *