EU watangaza kuongeza msaada wa kibinadamu katika kukabiliana na wimbi la wakimbizi wa Sudani

Umoja wa Ulaya utaongeza kwa kiasi kikubwa mchango wake katika shughuli za kibinadamu nchini Chad. Katika muktadha wa kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani na huku mzozo nchini Sudan ukikaribia miaka miwili, Chad inakabiliwa na wimbi kubwa la wakimbizi katika eneo la Ouaddaï, mashariki mwa nchi hiyo. Ingawa misaada ya Ulaya haiondoi pengo kwa msaada bada ya Marekani kusitisha misaada yake. Hata hivyo msaada wa Ualaya unakaribishwa katika nchi hii ya Toumaï.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum Adré, Victor Mauriat

Ni safari ya “ishara”, kulingana na Hadja Lahbib, Kamishna wa Ulaya. Mbele ya kituo cha mpaka cha Adré – ambapo kati ya wakimbizi 100 na 200 huingia kila siku kulingana na UNHCR – ametangaza mfuko mpya wa misaada ya kibinadamu ya Ulaya. “Tuko hapa kuchangia kifedha, kwa euro milioni 74,” anaeleza, “jambo ambalo litasaidia mashirika ya Umoja wa Mataifa, ambayo kwa bahati mbaya yanabidi kukabiliana na kupunguzwa kwa misaada ya kifedha ambayo hadi sasa imekuwa ikitolewa na wafadhili wengine, haswa Marekani.

Kwa upande wake, Zara Mahamat Issa, Waziri wa Chad wa anayehusika na masuala ya Kijamii, Mshikamano na Masuala ya Kibinadamu, amebainisha, licha ya matatizo, sera ya mapokezi inayofuatwa na Chad tangu mwanzo wa mzozo.  “Chad inashinda wimbi kubwa la wakimbizi, na hii inafanyika mfululizo,” anahakikisha. “Kwa sasa, kuna idadi kubwa ya wakimbizi, ambayo ninaweza kukadiria angalau watu 300,000 kwenye mpaka. Sasa kuna mazungumzo ya kuwahamisha kwenye kambi, hali ambayo inahitaji rasilimali nyingi.”

Kuelekea mkutano wa amani nchini Sudani

Baada ya kuondoka kuelekea Ndjamena siku ya Jumatano alasiri, Aprili 9, 2025, Hadja Lahbib atafanya mazungumzo ya ngazi ya juu katika mji mkuu wa Chad siku ya Alhamisi, kabla ya kuwakilisha Umoja wa Ulaya katika mkutano wa amani wa Sudani ulioandaliwa Aprili 15 mjini London.

Mkutano huu unaoongozwa na Ujerumani, Ufaransa, Uingereza na Umoja wa Ulaya, umekosolewa vikali na pande zinazopigana nchini Sudan, ikiwa ni pamoja na Vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) wala jeshi la kawaida la Sudan ambalo limealikwa.

Khartoum pia inalaani uwepo wa Umoja wa Falme za Kiarabu, unaoshutumiwa kwa kuipatia RSF silaha kupitia mashariki mwa Chad.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *