
Baraza la usalama la umoja wa Afrika limekutana jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kujadili mzozo unaoendelea nchini Sudan na mashariki ya DRC.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kikao hicho kilisimamiwa na rais mpya wa baraza hilo rais wa Equatorial Guinea Theodore Obiang Nguema ambayo amesisitiza haja ya usitishwaji mapigano hali ambayo imeathiri ukanda mzima wa Afrika.
Naye mwenyekiti anayeondoka wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki akisema suluhisho la kijeshi halina faida na haliwezi kufanya kazi barani Afrika.
Nchi husika kwenye mzozo huo, ziliwakilishwa na rais Paul Kagame wa Rwanda, DRC Waziri Mkuu Judith Suminwa na Sudan Waziri wa mambo ya nje.
Viongozi wengine walioshiriki kikao hicho ni katibu mkuu Antonio Guterres rais William Ruto, Samia Suluhu wa Tanzania.
Viongozi hao wa Afrika wanaokutana mjini Addis Ababa baadae leo Jumamosi wanatarajiwa kumchagua mwenyekiti mpya wa Tume ya AUC.
Ushindani mkali unatarajiwa kati ya mgombea wa Kenya, aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga, waziri wa mambo ya nje wa Djibouti Mahmoud Ali Youssouf na Richard Randriamandrato kutoka Madagascar.