Ethiopia: TPLF, chama cha kihistoria cha Tigray, chafutiwa usajili na Tume ya Uchaguzi

Chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF), ambacho kilitawala Ethiopia kwa takriban miongo mitatu, kinapoteza rasmi hadhi yake kama chama cha kisiasa. Katika uamuzi wake, Tume ya Uchaguzi ya Ethiopia ilitaja kushindwa kwake kuzingatia majukumu yake ya kisheria. Uamuzi uliopingwa na chama hicho.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Addis Ababa, Marlène Panara

Tume ya Uchaguzi ya Ethiopia imetangaza siku ya Jumatano, Aprili 14, kufutwa rasmi kwa chama cha TPLF (Tigray People’s Liberation Front) katika orodha ya vyama vya siasa nchini humo. Kutenguliwa huku kunatokana na uamuzei wa kuvunjwa kwa chama hiki ambao ulitekelezwa mwezi Februari mwaka huu, wakati TPLF iliposhindwa kuandaa mkutano mkuu, kama inavyotakiwa na sheria ya uchaguzi. “TPLF haijaheshimu masharti haya,” Tume inasisitiza katika taarifa yake.

TPLF yaomba makubaliano ya Pretoria

Kwa upande wake, TPLF inajibu kuwa Mkataba wa Pretoria, ambao ulimaliza vita vya Tigray mnamo mwezi Novemba 2022, unaiwezesha kusajiliwa kama chama cha siasa. “Kukataa kutambuliwa kwetu kisheria kunadhoofisha misingi ya makubaliano ya amani,” chama hicho kilibainisha wiki moja kabla ya kuvunjwa kwake. Utetezi uliotupiliwa mbali na Tume ya Uchaguzi, ukielezea hoja hiyo kuwa “isiyokubalika.”

Hii si mara ya kwanza kwa TPLF kutengwa na mchezo wa siasa. Mwishoni mwa mwaka wa 2020, mwanzoni mwa vita kati ya waasi wa Tigray na vikosi vya serikali, chama hiki kilikuwa tayari kimepoteza hadhi yake ya kisheria. Chama hiki kinaweza kutuma maombi ya kusajiliwa tena kama chama cha kisiasa kwa ajili ya uchaguzi wa Juni 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *