
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, amesema nchi yake haitafuti mzozo au adui wa muda mrefu na jirani yake nchi ya Eritrea kuhusu eneo la bahari Nyekundu, matamshi anayoyatoa baada ya maafisa wa ukanda na wataalam kuonya kuhusu uwezekano wa kutokea vita kati ya majirani hao wa Pembe ya Afrika.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Hofu ya kutokea mzozo kati ya nchi hizo iliibuka hivi karibuni baada ya Eritrea kuhamasisha raia Wake kujiunga na jeshi nchi nzima, ambapo pia kulingana na mashirika ya haki za binadamu, Ethiopia ilipeleka wanajeshi kwenye êneo la mpaka wa nchi hizo mbili.
Kupitia ukurasa Wake wa kijamii wa X, waziri mkuu Abiy Ahmed, amesema “Ethiopia haina nia yoyote ya kujihusisha na mzozo na Eritrea kwa madhumuni ya kupata êneo la bahari yake,”.
Nchi ya Ethiopia ambayo haina bahari, imekuwa ikitafuta kujenga bandari ya kimkakati kwa majirani zake, ambapo mwaka jana ilingia makubaliano na Somaliland, hatua iliyoibua mzozo kati yake na Somalia.