
Chama cha Ukombozi cha Watu wa Tigray, ambacho kinasimamia eneo la kaskazini mwa Ethiopia, kilishindwa kufanya mkutano wake mkuu, na kusababisha kusimamishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo. Mgawanyiko katika chama hicho uliosababishwa na mizozo, umeibua hofu ya kuzuka upya kwa mzozo katika eneo hilo.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Takriban wiki mbili zilizopita, nchini Ethiopia, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikisimamisha chama cha TPLF, Tigray People’s Liberation Front kwa muda wa miezi mitatu. Chama hiki kinasimamia eneo hili kaskazini mwa nchi, ambalo limeharibiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe dhidi ya serikali ya shirikisho.
Mkataba wa Pretoria, uliotiwa saini mwaka wa 2022, ulimaliza mzozo huu ambao uligharimu maisha ya watu karibu watu 600,000. Lakini leo TPLF imegawanyika. Mnamo mwezi wa Agosti, ilishindwa kuandaa mkutano wake mkuu, jambo ambalo lilisababisha kusimamishwa kwake.
“Mgogoro wa vizazi”
Kwa upande mmoja, msimamo mkali wa TPLF unafanywa na Gebremichael Debretsion, rais wa chama hicho. Kwa upande mwingine, wafuasi wa mwanamageuzi Getachew Reda, makamu wa rais wa zamani, ambaye kwa sasa ni mkuu wa TIRA, utawala wa muda wa kikanda wa Tigray. Ni nini kinachowatofautisha? “Mgogoro wa kizazi,” anabaini mmoha wa wajumbe wa chama hicho.
Kulingana na Gerrit Kurtz, mtafiti katika Taasisi ya Ujerumani ya Masuala ya Kimataifa, “uongozi wa TPLF unashukiwa kujaribu kukwepa uwajibikaji. Iwe ni ufisadi, makosa yake ya kisiasa au uhalifu uliofanywa wakati wa vita. “Kuhusu TIRA, inashtumiwa kuwa karibu sana na serikali ya shirikisho.
Mohamed Kheir Omer, mwandishi na mchambuzi wa kisiasa, anafuatilia masuala ya Ethiopia na Eritrea haswa. Anasema ugomvi wa ndani wa TPLF hauna dhamira ya kweli zaidi ya kugombea madaraka kati ya viongozi wa kisiasa. “Walikuwa na majadiliano marefu kwa miezi kadhaa, lakini hayakuwa mazungumzo kuhusu watu wa Tigray au juu ya watu hawa wote waliohamishwa ambao wanataka kurudi nyumbani. Ilikuwa tu kuhusu mamlaka, huku kila mmoja wao akidai kuwa kiongozi halali,” mchambuzi huyo anaeleza.
Kuna hatari ya kuanza tena kwa migogoro?
Leo, ucheleweshaji wa utekelezaji wa makubaliano ya amani ya Pretoria unazidisha mvutano. Wanamgambo wa Amhara na wanajeshi wa Eritrea bado wapo Tigray. Upokonyaji silaha umekwama na takriban watu milioni moja waliokimbia makazi yao bado hawajarejea nyumbani.
Wakati huo huo, waangalizi wanahofia kuanza tena kwa mzozo huo, kiasi kwamba ujumbe wa wanadiplomasia sita wa Marekani na Ulaya ulikwenda wiki hii Mekele, mji mkuu wa Tigray.