Esther Chabruma: Ubingwa bado kabisaaa!

KOCHA wa JKT Queens, Esther Chabruma amesema msimu huu huenda bingwa akatokea mwisho wa msimu kutokana na ushindani uliopo kwenye ligi hiyo.

Huu ni msimu wa pili kwa Chabruma kusimama kama kocha mkuu wa JKT, baada ya mwaka jana kupoteza ubingwa mbele ya Simba.

Akizungumza na Mwanaspoti, Chabruma alisema ligi msimu huu imekuwa na ushindani na akatoa msisitizo kwamba watu wasishangae bingwa akatangazwa kwenye mechi za mwisho.

Aliongeza kuwa msimamo wa ligi ulivyo unaonyesha namna gani bado kuna kazi ya kufa au kupona kwenye mechi tano zilizosalia zitakazomtangaza bingwa.

“Tofauti na msimu uliopita huu ni mgumu na mwaka hu timu zimejipanga umeona hata kwenye mechi ya dabi, watu walizoea kuiona zikicheza timu hizo, Simba inashinda lakini sasa mambo yamebadilika,” alisema Chabruma na kuongeza:

“Unaweza kusema umebakiza mechi mbili ngumu, Simba na Yanga ukaja kupoteza mechi na timu ndogo kwa sababu wanapocheza na timu kubwa huonyesha uwezo wao.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *