Eslami: Upande wa Ulaya umeiambia Iran kuwa ‘uondoaji vikwazo hauko kwenye mamlaka yetu’

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran, amesema kuhusu mazungumzo yaliyofanywa kati ya Jamhuri ya Kiislamu na Ulaya kwamba, maelezo ya msingi ya upande wa Ulaya ni kuwa ‘vikwazo haviko mikononi mwetu, hatuna nafasi yoyote juu ya suala hilo na kadhia hii iko kwenye mamlaka ya Marekani’.