Equatorial Guinea yakanusha kuwatuma vijana wa Equatorial Guinea kwenda vitani nchini Ukraine

Makamu wa rais wa Equatorial Guinea amekanusha kwenye mtandao wa kijamii wa X ripoti ya vyombo vya habari kwamba vijana wa Equatorial Guinea walikuwa wakitumwa kwenda vitani nchini kusaidia jeshi la Urusi.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

“Ningependa kukanusha taarifa kuhusu kutumwa kwa wanajeshi wa Equatorial Guinea nchini Urusi kupigana nchini Ukraine; ni uongo mtupu,” ameandika Teddy Nguema, makamu wa rais wa nchi hii ndogo inayozungumza Kihispania katika Afrika ya Kati.

Kulingana na gazeti la mtandaoni la Diario Rombe lenye makao yake nchini Uhispania, ambalo liko karibu na upinzani wa Equatorial Guinea, makubaliano ya kijeshi kati ya Moscow na Malabo ni pamoja na harakati za kuajiri watu kwa ajili ya mzozo wa Ukraine.

Si kweli, anaandika makamu wa rais wa Equatorial Guinea. Kulingana na Equatorial Guinea, vijana wa Equatorial Guinea wanaokwenda Urusi “hawaendi vitani, lakini wanapata mafunzo katika vyuo vikuu vya kifahari vya Shirikisho la Urusi. Baada ya kumaliza masomo yao, wanarudi nchini kwa fahari ili kuchangia ulinzi wa nchi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *