Emmanuel Macron: Ufaransa na Canada ni ‘chi za amani”‘na zinadai ‘ahadi za wazi’ kutoka Urusi

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza siku ya Jumatatu, Machi 17, kwamba Ufaransa na Canada ni “nchi za amani” na “washirika wa kutegemewa” ambao wataendelea kudai “ahadi za wazi” kutoka kwa Urusi kwa “amani ya kudumu” nchini Ukraine na “usalama wa Ulaya nzima.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

” Canada na Ufaransa zinataka “amani thabiti na ya kudumu, ikiambatana na dhamana dhabiti ambayo itailinda Ukraine dhidi ya uvamizi wowote mpya wa Urusi na kuhakikisha usalama wa Ulaya nzima,” ametangaza rais wa Ufaransa pamoja na Waziri Mkuu mpya wa Canada Mark Carney katika Ikulu ya Élysée. “Ni kwa nia hii ambapo tutadumisha uungaji mkono wetu kwa Ukraine na kuendelea kudai ahadi za wazi kutoka kwa Urusi,” ameongeza.

Waziri Mkuu mpya wa Canada, Mark Carney, amesema anataka kuimarisha uhusiano wa nchi yake na “washirika wa kutegemewa” barani Ulaya wakati ambapo Canada iko chini ya shinikizo la kibiashara kutoka kwa Marekani na vitisho vya mara kwa mara vya unyakuzi kutoka kwa Donald Trump. “Ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kuimarisha uhusiano na washirika wa kuaminika kama Ufaransa,” amesema akiwa pamoja na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa ziara yake ya kwanza nje ya nchi. “Sote tuko kwa ajili ya uhuru na usalama, kama inavyoonyeshwa na uungaji mkono wetu usioyotetereka kwa Ukraine,” ameongeza.

Waziri Mkuu mpya wa Canada, Mark Carney, amechagua Ufaransa na Uingereza kwa ziara yake ya kwanza rasmi nje ya nchi. Yuko Paris leo Jumatatu, Machi 17. Chaguo hili la kimkakati linatuma ujumbe mzito: Canada inataka kubadilisha miungano yake na kuimarisha uhusiano wake na Ulaya, ikitegemea washirika hawa wawili wa kihistoria.

Kisha ataelekea London kesho Jumanne kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer. Mkutano na Mfalme Charles III pia umepangwa katika upande wa pili wa Manche, nchini Uingereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *