
Licha ya tofauti kubwa katika suala hilo, Donald Trump na Emmanuel Macron wamehakikisha siku ya Jumatatu Februari 24 kwamba wanataka kufanya kazi pamoja kumaliza vita vya Ukraine, miaka mitatu baada ya kuanza kwa mashambulizi ya Urusi.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Rais wa Ufaransa, aliyepokelewa na mwenzake wa Marekani katika ikulu ya White House, ameahidi majadiliano kwa nia ya amani “ya kudumu” na anatumai ushiriki “mkubwa” wa Marekani katika suala hili. Donald Trump, wakati wa kipindi cha maswali na majibu na waandishi wa habari, amejivunia uhusiano wake “maalum” na mwenzake wa Ufaransa, na akahakikisha kwamba anaweza kumaliza uhasama katika “wiki chache.”
Rais wa Marekani pia ameona kwamba kutiwa saini kwa makubaliano na Ukraine kuhusu upatikanaji wa madini ya Marekani nchini humo ni hatua ambayo “inakaribia”, na hata akataja ziara ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika Ikulu ya White House ili kuidhinisha mkataba huo, “wiki hii au ijayo”. Anaiona kama njia kwa Marekani kurejesha gharama iliyotumika katika kuisaidia kijeshi Kyiv tangu mashambulizi ya Urusi mwaka 2022.
Donald Trump, ambaye anahesabu zaidi juu ya mazungumzo yake na Rais wa Urusi Vladimir Putin kusitisha mapigano, pia amesema kwamba wa rais Putin atakubali kutumwa kwa wanajeshi wa Ulaya nchini Ukraine, lakini ameedelea kukwepa dhamana ya usalama ambayo Washington inaweza kuwapa wanajeshi hao. “Nchi za Ulaya ziko tayari kupeleka wanajeshi” ili kuthibitisha kwamba “amani inaheshimiwa,” amesema Emmanuel Macron, pia akihakikisha kwamba Ulaya iko tayari “kuimarisha” ulinzi wake.
Trump na Macron watofautiana
Ikiwa Emmanuel Macron amezungumza na Donald Trump kuhusu Urusi kama “mchokozi” wa Ukraine, rais wa Marekani anaendelea kuziweka nchi hizo mbili katika ngazi moja, wakati hajamshtumu Volodymyr Zelensky kuhusika kwa mzozo huo, kama alivyofanya hivi karibuni. Emmanuel Macron amesema “anashawishika kwamba kulikuwa na njia” na Donald Trump kumaliza vita nchini Ukraine.
Hata hivyo, rais wa Ufaransa amebaini kwamba makubaliano ya amani hayawezi kumaanisha “kutekwa” kwa Kyiv, na amesisitiza juu ya haja ya kutoa “dhamana ya usalama” ili kumzuia rais Vladmir Putin kufanya tea mashambulizi. “Tunataka mpango wa haraka, lakini sio ambao ni dhaifu,” rais wa Ufaransa amesema.
Sambamba na mkutano wa Washington, Marekani na nchi za Ulaya walikabiliana katika Umoja wa Mataifa. Marekani, kama Urusi, ilipiga kura dhidi ya azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kuthibitisha kuunga mkono Ukraine na uadilifu wake wa eneo.
Rais wa Ufaransa alishiriki siku ya Jumatatu asubuhi na mwenzake wa Marekani katika mkutano wa video wa viongozi wa G7. Viongozi kadhaa wa kigeni walikusanyika katika mji mkuu wa Ukraine ili kuonyesha mshikamano wao na Volodymyr Zelensky, ambaye alipongeza “miaka mitatu ya upinzani.”
Kujaribu kumshawishi Donald Trump
Akivunja sera ya mtangulizi wake Joe Biden ya uungwaji mkono mkubwa kwa Kyiv, Donald Trump ameamua kwamba mtu anayepewa nafasi kubwa ni Rais wa Urusi Vladimir Putin. Emmanuel Macron mwenyewe alisema siku ya Jumatatu kwamba Ukraine ilibidi “ihusishwe” katika mazungumzo hayo, wakati ambapo nchi za Ulaya zinahofia kutekwa kwa Kyiv na Washington na Moscow.
Miaka mitatu baada ya kujaribu bila mafanikio kumzuia Vladimir Putin kushambulia Ukraine, Emmanuel Macron ameanza kazi isiyo na uhakika sawa na rais wa Marekani. Anataka kumshawishi mwenzake wa Marekani, ambaye hajawahi kuficha kuvutiwa kwake na viongozi wa kimabavu, kwamba Urusi ni “tishio lililopo” na kwamba Vladimir Putin “hataheshimu” usitishaji mapigano.