
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza siku ya Alhamisi Machi 20 kwamba mkutano mpya utafanyika Alhamisi ya wiki ijayo huko Paris na Volodymyr Zelensky na washirika wa Ukraine. “Tumefanya kazi nyingi na Waingereza kwa masharti ya kusimamia usitishaji vita, na kwa hivyo nadhani hii itakuwa fursa ya kujadili hali hii na kutoa ufafanuzi,” rais wa Ufaransa ametangaza.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Rais Emmanuel Macron ametangaza siku ya Alhamisi, Machi 20, kwamba mkutano mpya utafanyika Machi 27 huko Paris na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na washirika wa Ukraine, “kukamilisha” hasa “uungaji mkono wa muda mfupi kwa jeshi la Ukraine.”
“Alhamisi ya wiki ijayo, tutafanya mkutano wa muungano wa walio tayari,” nchi zilizo tayari kuchangia kwa njia moja au nyingine “dhamana ya usalama” kwa Ukraine kama sehemu ya uwezekano wa makubaliano ya amani, rais wa Ufaransa ametangaza baada ya mkutano wa baraza la Umoja wa Ulaya huko Brussels.
“Lengo langu hapo siku ya Alhamisi, kwanza kabisa ni kuhakikisha kuwa kuna dhamira iliyorudiwa na ya wazi, na labda maalum zaidi, kuhusu msaada wa muda mfupi kwa Ukraine,” amesema.
Mkutano huo mpya unaofuatia mikutano kadhaa mjini Paris na London tangu mwanzoni mwa mwezi Machi, utakuja baada ya mazungumzo yanayoongozwa na Marekani na Urusi na Ukraine yenye lengo la kupata usitishwaji wa mapigano usio kamili, yaliyopangwa kufanyika Jumatatu nchini Saudi Arabia.
Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer wamekuwa wakijaribu kuweka pamoja muungano huu wa nchi zinazounga mkono Ukraine tangu Rais wa Marekani Donald Trump alipofungua mazungumzo ya moja kwa moja na Urusi mwezi uliopita katika jitihada za kumaliza miaka mitatu ya vita.
“Siko kichwani mwake.”
“Tumefanya kazi nyingi na Waingereza kwa masharti ya kusimamia usitishaji vita, na kwa hivyo nadhani hii itakuwa fursa ya kujadili hali hii na kutoa ufafanuzi,” rais wa Ufaransa ametangaza.
“Lengo linalofuata ni kufafanua viwango tofauti vya uungaji mkono kwa Ukraine baada ya amani, kwa jeshi la Ukraine na lile la uwezekano wa kutumwa kwa wanajeshi,” ameongeza.
Kulingana na Emmanuel Macron, “majibu ya kiasi na ya kukatisha tamaa ya Urusi” kwa pendekezo la Marekani na Ukraine la usitishwaji kamili wa mapigano wa mwezi mmoja “linasema jambo ambalo tumekuwa tukilaani kwa miezi kadhaa: kwamba Urusi haitaki amani hii kwa dhati katika hatua hii.”
Ni nini kinachoweza kuathiri msimamo wa Rais wa Urusi Vladimir Putin? “Mumulize! Siko kichwani mwake. Kwa njia moja , kwa bahati nzuri,” rais wa Ufaransa amesema. “Lakini nadhani kwamba kwanza kabisa, tunachohitaji kufanya ni kuonyesha dhamira yetu (…) kwa Waukraine,” ameongeza.