
Jumuiya ya ECOWAS imeelezea kuguswa na mzozo unaoendelea kati ya nchi ya Algeria na jirani yake nchi ya Mali.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Tangazo la ECOWAS limekuja baada ya Jumatatu ya wiki hii, utawala wa Algiers na ule wa Bamako, kila mmoja kutangaza kuzuia anga yake kutumiwa na mwingine kufuatia mzozo wa kudunguliwa kwa ndege isiyo na rubani ya Mali.
Katika taarifa yake, ECOWAS inasema inaguswa na mzozo baina ya nchi hizo mbili, ikitoa wito kwa viongozi wa nchi hizo kuketi kwa mazungumzo ili kumaliza tofauti zao.
Juma lililopita Algeria ilitangaza kudungua ndege isiyo na rubani ya mali iliyokuwa inafanya doria kwenye mpaka wa nchi hizo, hatua ambayo iliikasirisha Mali iliyojibu kwa kumrejesha nyumbani balozi wake pamoja na kuutuhumu utawala wa Algiers kufadhili magaidi wanaotatiza usalama wake.
Aidha katika kile kinaonekana kuendelea kuzorota kwa uhusiano wao, Algeria ilitangaza kuzuia anga yake kutumiwa na ndege kutoka au zinazoingia Mali, uamuzi uliojibiwa sawia na utawala wa Bamako.