
Idadi ya watu walionyongwa kote duniani iliongezeka hadi zaidi ya 1,500 mwaka wa 2024, hii ikiwa idadi ya juu zaidi kuwai kurekodiwa kulingana na ripoti ya shirika la Amnesty International.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Huku baadhi ya mataifa yakikataa kutoa ripoti kamili ya watu walionyongwa, shirika la Amnesty International linasema kuwa idadi hii bado ni ndogo.
Mataifa ya Iran, Saudia Arabia na Iraq zimechangia 90% ya visa kesi zilivyoripotiwa huku Saudi Arabia ikiongeza idadi yake maradufu.
Amnesty International, hata hivyo, iliitaja China kama taifa lenya idadi kubwa zaidi ya visa vya unyongaji kila mwaka, huku ikiishuku Korea Kaskazini na Vietnam kwa kutumia sana hukumu ya kifo.
Licha ya ongezeko la kutisha la mauaji mwaka 2024, ni nchi 15 pekee ndizo zilizotekeleza hukumu ya kifo kwa mwaka wa pili mfululizo ambapo idadi hiyo imekuwa ndogo.
Aidha jumla ya nchi 145 sasa zimefutilia mbali hukumu ya kifo kisheria. Na kwa mara ya kwanza, theluthi mbili ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa walipiga kura ya kuunga mkono kusitishwa kwa matumizi ya hukumu ya kifo.