DRC:Waziri Mkuu wa zamani Matata Ponyo ahukumiwa miaka 10 ya kazi ya kulazimishwa

Mahakama ya Katiba nchini DRC imemhukumu siku ya Jumanne, Mei 20 kiongozi wa upinzani na Waziri mkuu wa zamani Augustin Matata Ponyo (2012-2016) kifungo cha miaka 10 ya kazi ya kulazimishwa, kwa ubadhirifu wa zaidi ya dola milioni 245 zilizokusudiwa kwa mradi wa bustani ya kilimo ya Bukangalonzo, nje ya mji mkuu Kinshasa.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa

Washirika wake walioko kwa sasa nje ya nchi: Gavana wa zamani wa Benki Kuu Deogratias Mutombo na mfanyabiashara kutoka Afrika Kusini Christo Grobler wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela. Huu ndio mwisho wa sakata ya kisheria ambayo imekuwa na misukosuko kadhaa tangu kufunguliwa kwake mnamo mwaka2021.

Miaka kumi gerezani kutekelezwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na miaka mitano ya kunyimwa kufikia nyadhifa za umma, haki ya kupiga kura na kuachiliwa kwa masharti. Hii ni chini ya miaka 20 ya kifungo iliyoombwa na mwendesha mashtaka.

Mahakama imehitimisha kuwa Augustin Matata Ponyo “amebuni, kushiriki na kufaidika” kutokana na ubadhirifu huo kwa kuthibitisha malipo yaliyozidishwa na kazi ambayo haikutekelezwa. Zaidi ya dola milioni 156 zilitengwa kwa bustani ya kilimo na dola milioni 89 kwa ujenzi wa soko la kimataifa mjini Kinshasa, miradi miwili ambayo haikuzaa matunda. Mahakama ilisisitiza kuwa Augustin Matata Ponyo alinyakua madaraka ya Waziri wa Fedha ambayo alikuwa akishikilia kabla ya kuwa Waziri Mkuu. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mahakama imeagiza kutaifishwa kwa mali za watu hao watatu kulingana na kiasi cha fedha zilizofujwa.

Hukumu iliyochukuliwa kuwa “ya upendeleo” na “isiyo ya haki” na utetezi wa Augustin Matata Ponyo. Wakili Laurent Onyemba amesema anasubiri idhini kutoka kwa mteja wake ili kupinga uhalali wa hukumu hii mbele ya majaji hao. Bw. Laurent Onyemba amesema: “Kulikuwa na kila kitu isipokuwa sheria. Ni muunganiko wa ukweli uliojitenga wa sheria. Uamuzi huo umetenganishwa na ukweli na unabatilisha uaminifu wowote kwa taswira ya vyombo vyetu vya sheria. Tutawasilisha, ikiwa wateja watakubali, ombi la ukiukwaji wa katiba kwa hukumu. Tuna hakikisho kwamba uamuzi huu ni wa kisiasa kwetu. “

Ikiwa Augustin Matata Ponyo bado yuko huru asubuhi ya leo, akionyesha kinga yake kama mbunge wa kitaifa. Ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma katika mahakama hii kuu inaweza hivi karibuni kutoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu huyo wa zamani.

Inabakia kuonekana iwapo hatatetewa na Bunge ambalo lilikuwa tayari limepinga kuendelea kwa kesi hii bila Mahakama ya Katiba kuomba kuondolewa kwa kinga za wapinzani.

Watu wengine wawili waliohukumiwa katika kesi hii wako nje ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *