
Watu zaidi ya 100 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na mafuruko na wengine mamia kupoteza makazi yao katika vijiji vilivyoko jirani na ziwa Tanganyika, mashariki mwa nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mafuriko yameathiri pakubwa kijiji cha Kasaza kilichoko wilayani Fizi, jimbini Kivu Kusini, tukio linaloripotiwa wakatik huu eneo la mashariki likishudia hali tete ya usalama kutokana na uvamizi wa waasi wa M23.
Mamlaka zinasema njia pekee ya kufikia kijiji hicho ni kupitia ziwa Tanganyika, Sammy Kalonji ni msimamizi wa wilaya ya Fizi.
‘‘Zaidi ya watu 100 ndio walishaonekana, nyumba kadhaa zikiharibiwa pamoja na wetu wengine kujeruhiwa.’’ Alisema Sammy Kalonji ni msimamizi wa wilaya ya Fizi.
Kwa upande wao mashirika ya kiraika yanatoa wito wa misaada yakibinadamu kufikishwa haraka kwenye eneo hilo ili kunusuru maisha ya raia.
Jacques Almasi ni msimamizi wa asasi za kiraia wilayani Fizi.
‘‘Serikali ya DRC na baadhi ya wasaidizi waje kuwasaidia watu kwa sababu shamba zimeharibiwa na maji.’’ Alisema Jacques Almasi ni msimamizi wa asasi za kiraia wilayani Fizi.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, serikali ya jimbo la Kivu Kusini iliyoko Uvira imesema tayari imetuma ujumbe wa dharura kwenye eneo la maafa ili kutathmini hali ya mambo.