
Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imetangaza siku ya Alhamisi, Mei 15, kuwa imewahamisha zaidi ya wanajeshi 1,300 wa Kongo na maafisa wa polisi kutoka mji wa mashariki wa Goma, ambao unadhibitiwa na kundi la waasi la M23.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mji wa mashariki wa Goma ulitekwa na kundi la waasi la M23 mwezi Januari. Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imesema operesheni hiyo ilikuwa “tata” na inahitaji mazungumzo marefu na MONUSCO, serikali na M23, ambayo imekataa uhamishaji kupitia uwanja wa ndege wa Goma, ambao umefungwa tangu udhibitiwe na waasi.
Kundi la M23, ambalo wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanasema linaungwa mkono na Rwanda, lilitwaa udhibiti wa Goma mwezi Januari, na kuashiria wimbi la hivi punde la ghasia katika mzozo wa miongo kadhaa mashariki mwa DRC.
Maelfu ya watu wameuawa katika mapigano hayo na karibu polisi na wanajeshi 2,000 wa serikali wamekimbilia katika kambi za kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO), kulingana na vyanzo vya Umoja wa Mataifa.
ICRC ilitangaza mwishoni mwa mwezi Aprili kuzinduliwa kwa misheni ya kusindikiza vikosi vya usalama kutoka Goma, katika safari ya kilomita 2,000 (maili 1,250) hadi mji mkuu, Kinshasa.
ICRC imesema “imewasindikiza” watu 1,359 wasiokuwa na silaha kutoka vikosi vya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na familia zao kati ya Aprili 30 na Alhamisi.
Mamia ya vikosi vya usalama wamejiunga na M23 au walikimbia kambi zao tangu mwezi Januari, kulingana na vyanzo vya Umoja wa Mataifa.
ICRC imesema operesheni hiyo ilikuwa “tata” na ilihitaji mazungumzo marefu na MONUSCO, serikali na M23, ambayo ilikataa uhamishaji wowote kupitia uwanja wa ndege wa Goma, ambao umefungwa tangu udhbitiwe na waasi hao.