DRC: Zaidi ya wagonjwa 800 wa kipindupindu warekodiwa tangu mwanzoni mwa mwaka Kalemie

Eneo la afya la Kalemie katika mkoa wa Tanganyika linakabiliwa na mlipuko wa kipindupindu. Tangu kuanza kwa mwaka huu, zaidi ya wagonjwa 800 wamerekodiwa, vikiwemo vifo 8, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa siku ya Ijumaa , Mei 16, na Germain Kalunga, msimamizi wa afya ya msingi (PHC) mkoani humo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Germain Kalunga anaeleza kuwa mlipuko huu wa kipindupindu umechangiwa kwa kiasi kikubwa na mafuriko ya hivi karibuni yaliyosababisha uchafu wa vyoo kutupwa katika Ziwa Tanganyika na Mto Lukuga. Sehemu ya raia hutumia maji haya machafu. Hata hivyo, ukosefu wa maji ya kunywa kutoka kwenye bomba, yanayotolewa na mamlaka ya maji, REGIDESO, unazidisha kudorora kwa hali ya afya.

“Tangu wiki ya pili ya mwaka huu, tayari tumekuwa katika janga la ugonjwa. Kuanzia Aprili 28, kulikuwa na ongezeko jipya la wagonjwa, pamoja na wagonjwa wapya 70, 80, au hata 100 kwa siku. ” Hali hii inatikisa jiji zima,” Germain Kalunga anaeleza, akinukuliwa na Radio OKAPI.

Kutokana na kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya wonjwa, vituo vya afya huko Kalemie vimezidiwa. “Tumezidiwa. Tumechukua hatua za kuwahudumia wagonjwa. Katika miezi minne, tangu kuanza kwa ugonjwa huu, tumerikodi  zaidi ya wagonjwa 838 na vifo 8 kwa bahati mbaya,” anaongeza.

Ili kukabiliana na mzozo huu, mamlaka ya afya imewataka haraka wauguzi wote wa jiji kuhakikisha huduma kwa wagonjwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *