DRC: Zaidi ya visa 100 vya kipindupindu vyarekodiwa ndani ya wiki moja Tanganyika

Mkoa wa Tanganyika, nchini DRC, unakabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu, huku zaidi ya wagonjwa 100 wakirekodiwa tangu mwanzoni mwa wiki hii katika maeneo ya afya ya Nyemba na Kalemie. Vifo viwili pia vimeripotiwa. Hali hii imebainishwa Jumamosi Mei 3, na Mkuu wa Ofisi ya Habari na Mawasiliano katika kitengo cha afya cha mkoa wa Tanganyika Dk.Wilma Lwabola.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Dk.Wilma Lwabola, akinukuliwa na Radio Okapi, kukatika kwa huduma ya maji ya kunywa ni moja ya sababu kuu zilizochangia mlipuko huu wa kipindupindu. Anafafanua:

“Mkoa wetu ulipata tatizo la maji, tatizo la upatikanaji wa maji ya kunywa kwa muda wa takribani siku 7. Imebainika kuwa kwetu sisi ni tatizo kubwa kuliko mipuko wa kipindupindu. Mkoa wetu ni janga tupu hasa kwa maeneo mawili ya afya yaliyopo katika jiji na wilaya ya Kalemie na Nyemba. Ugonjwa wa Kipindupindu ni cha kudumu unaendelea kuwepo, lakini kuna sababu zinazochangia au kuzidisha ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maji safi na maji ya REGIDESO. “

Kutokana na uhaba huu wa maji ya kunywa, wakazi wa eneo hilo wamegeukia vyanzo vya maji ambayo hayajasafishwa, kama vile Mto Lukuga na Ziwa Tanganyika, ambako maji hayana klorini. Hali hii imechangia kuenea kwa kasi kwa ugonjwa huo.

Kuongezeka kwa kasi kwa wagonjwa

Mlipuko huo ulianza Aprili 29, na takwimu zinaonyesha kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa, hali inayotia wasiwasi Dk. Lwabola anaeleza:

“Kuanzia siku ya Jumatatu, tulikuwa na kesi nyingi mpya: tulifikia kesi mpya 79 kwa siku moja tu, na siku ya Jumanne, tulikuwa na kesi 39. Leo, tangu tufanye mkutano, tuna kesi 18 tangu asubuhi.”

Hali katika maeneo ya afya ya Nyemba na Kalemie inatia wasiwasi hasa, kwani maeneo haya yanachukuliwa kuwa janga la kawaida, ambapo kipindupindu kinaendelea kuwepo lakini idadi ya wagonjwa inaweza kuwa kubwa kutokana na sababu mbalimbali zinazozidisha hali hiyo. Mamlaka ya afya  hatua za haraka zichukuliwe kurejesha usambazaji wa maji ya kunywa na kuimarisha hatua za kuzuia, ikiwa ni pamoja na uwekaji wa klorini katika maji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *