DRC yawapandisha kizimbani wanajeshi wake kwa kutoroka vita; inawatuhumu pia kwa ubakaji

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza kuwa wanajeshi wasiopungua 75 wanatazamiwa kufikishwa mahakamani leo Jumatatu wakikabiliwa na shtaka la kuwakimbia wapiganaji wa kundi la waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda katika jimbo la Kivu ya Mashariki ya Kivu.