
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imetangazwa kuwa inastahiki siku chache zilizopita kwa Hazina ya Kujenga Amani kwa kipindi cha miaka mitano, kuanzia mwaka 2025 hadi mwaka 2029.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alimfahamisha Rais wa Jamhuri kuhusu hilo katika barua iliyotumwa kwa Radio Okapi siku ya Jumamosi, Aprili 12, kulingana na radio hiyo.
Antonio Guterres alikuwa akijibu ombi ambalo Rais Félix Tshisekedi alilomuomba Desemba mwaka jana.
“Kupitia msaada huu, Mfuko utaendelea na ahadi yake pamoja na Serikali ya Kongo ya kuimarisha uwezo wa kitaifa wa kujenga amani, kuhakikisha kuwa mafanikio yaliyopatikana yanadumishwa. “Msaada huo utatekelezwa kupitia mipango inayoongozwa na timu ya Umoja wa Mataifa na washirika wake, kwa kuzingatia Mfumo wa Ushirikiano Endelevu wa Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha mwaka 2025-2029,” Antonio Guterres.
Kwa mzunguko huu mpya, nyanja tatu zinazopewa kipaumbele zimethibitishwa na Kamati ya Uongozi ya PBF, hususan:
- Kuimarisha utawala na uwiano wa njia za kujenga amani na kuzuia migogoro;
- Kusaidia ustahimilivu wa jamii na watu walio hatarini zaidi kukabiliwa na migogoro, kwa kuendeleza masuluhisho endelevu na kushughulikia sababu za msingi, hasa zile zinazohusishwa na maliasili, madini na ardhi;
- Kuimarisha ulinzi wa raia, usalama, haki za binadamu na vyombo vya sheria, ikiwa ni pamoja na haki ya mpito, kwa nia ya mpito inayohusishwa na kujiondoa taratibu na kuwajibika kwa MONUSCO.
Kwa mujibu wa utaratibu wa kawaida wa Hazina hii, mipango mipya itatambuliwa hatua kwa hatua, kulingana na mgao wa kila mwaka unaowasilishwa na Ofisi ya Usaidizi wa Ujenzi wa Amani (PBSO) huko New York.
Juhudi hizi zitawekwa chini ya uangalizi wa wenyeviti wenza wa Kamati ya Kitaifa ya Uongozi ya PBF nchini DRC, kwa msaada wa Sekretarieti ya Pamoja ya PBF yenye makao yake makuu mjini Kinshasa.
Upyaji huu unaashiria hatua mpya katika ushirikiano kati ya Serikali ya Kongo na Umoja wa Mataifa katika suala la ujenzi wa amani nchini DRC.
PBF, mfumo wa ufadhili wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, unalenga kusaidia ujenzi wa amani duniani kote. Nchini DRC, tangu mwaka 2009, afua za Hazina zimesaidia uimarishaji wa utawala, uwiano wa taratibu za kujenga amani na kuzuia migogoro.
Kwa Mfumo wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, “kustahiki tena kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa Hazina ya Kujenga Amani ni ishara dhabiti, inayoangazia umuhimu wa kuzingatia hasa eneo hili katika mazingira magumu ya kifedha ya kimataifa,” amesema Adama Moussa, Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini DRC.
Kuridhika kwa Serikali ya Kongo
Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Mipango na Uratibu wa Misaada ya Maendeleo amekaribisha hatua hiyo akisisitiza kuwa mzunguko huu mpya unalenga kuimarisha ufanisi wa mifumo iliyopo na kuiunga mkono serikali katika jitihada zake za kuzuia ghasia na migogoro.
Wakati wa mzunguko uliopita (2019-2024), ikiwa na miradi 22 iliyofadhiliwa kwa Dola za Kimarekani milioni 49, PBF ilisaidia shughuli katika mikoa ya Kasai, Kasai ya Kati, Kivu Kusini na Tanganyika, kwa kupendelea utangamano wa kijamii, utawala wa ndani unaojumuisha, ujumuishaji wa jamii, kuzuia migogoro na mpito unaohusishwa na kuondoka kwa MONUSCO hatua kwa hatua.