DRC: Waziri Mkuu Suminwa kumwakilisha rais Thisekedi Addis Ababa

Waziri Mkuu wa DRC Judith Suminwa Tuluka yuko jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kumwakilisha rais Felix Thisekedi katika baraza la usalama na amani la Umoja wa Afrika.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Waziri Suminwa anatarajiwa kuzungumzia uvamizi wa Rwanda na changamoto ya usalama mashariki ya DRC na kushinikiza kuondolewa kwa wanajeshi wa Rwanda kwenye ardhi ya Kongo.

DRC inasisitiza kuondolewa mara moja kwa wanajeshi wa Rwanda kwenye ardhi yake pamoja na kuheshimiwa uhuru wa ardhi ya Kongo.

Kulingana na DRC zaidi ya watu Elfu tatu wamefariki wakati maelfu ya wengine wakiwa wamepoteza makazi yao mjini Goma, Mji Mkuu wa Kivu Kaskazini katika mashambulio ya makundi ya waasi.

Umoja wa Mataifa na Mataifa ya Magharibi yameituhumu nchi ya Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23, serikali ya DRC ikitaka Rwanda na waasi wa M23 kuekewa vikwazo kwa ukiukaji wa haki za binadamu na uhuru wa ardhi ya Kongo.