DRC: Watu milioni 28 wako katika uhaba mkubwa wa chakula nchini

Nchini DRC, hali ya utapiamlo imezorota katika miezi ya hivi karibuni, kulingana na makadirio kutoka Ainisho ya Awamu ya Usalama wa Chakula Iliyounganishwa (IPC). Kulingana na shirika hilo, karibu Wakongo milioni 80 wameathiriwa na hali ya uhaba wa chakula na milioni 28 wanahitaji hatua za haraka.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Kinshasa, Paulina Zidi 

Kutokana na mzozo wa sasa unaoathiri DRC, IPC imelazimika kurekebisha makadirio yake kwenda juu. Mnamo mwezi Oktoba 2024, mpango huu wa wadau mbalimbali unaolenga kuboresha uchambuzi na kufanya maamuzi katika usalama wa chakula na lishe ulikadiria kuwa karibu watu milioni 25 watakuwa katika hali ya uhaba mkubwa wa chakula nchini mwaka wa 2025. Hatimaye, ni karibu milioni 28, idadi ambayo ni kusema karibu mtu mmoja kati ya wakazi wanne.

Shirika hilo linaonya kwamba ikiwa hakuna kitakachofanyika, takwimu hii inaweza kuendelea kuongezeka na ukosefu wa chakula na lishe wa watu unaweza kuzorota zaidi.

Takriban watu milioni 51 wako katika hali ya mkazo wa chakula, kiwango ambacho kinatangulia dharura. Hali ambayo inaathiri takriban mikoa yote ya nchi, sio tu ile iliyo katika vita. Zaidi ya 34% ya wakazi wa Tanganyika wana uhaba mkubwa wa chakula, 29% kwa wale wa Kasai ya Kati.

Mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu hayana matumaini kwa miezi ijayo. “Programu kadhaa za kukabiliana na utapiamlo kwa sasa zimesimama kutokana na kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani,” anasema mmoja wa viongozi hao wa mashirika ya kihisani, akionya kuwa ufadhili wa Ulaya hautatosha kuziba pengo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *