
Kwa mara ya kwanza baada ya mwaka mmoja, Félix Tshisekedi na Paul Kagame, marais wa Kongo na Rwanda, walikutana mjini Doha mapema wiki hii. Mkutano huo wa ana kwa ana, ambao ulifanyika siku ya Jumanne, Machi 18, kwa jitihada za Amir wa Qatar na ulilenga kutafuta suluhu la mzozo wa usalama mashariki mwa DRC. Lakini mjini Kinshasa, mkutano huo unatatizika kushawishi sehemu ya upinzani.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Kinshasa, Paulina Zidi
Siku moja baada ya mkutano kati ya Felix Tshisekedi na Paul Kagame huko Doha siku ya Jumanne, Machi 18, sehemu ya upinzani wa Kongo, hawana imani na mkutano huo, na wana mashaka juu ya mkutano huu wa ana kwa ana kati ya viongozi hao wawili.
“Mkutano huu ulishangaza wengi,” anaeleza Prince Epenge, kutoka muungano wa Lamuka unaoongozwa na Martin Fayulu. “Tuna hakikisho gani kwamba mikutano hii nchini Qatar haitasababisha hali kuwa mbaya zaidi?” anauliza msemaji wa upinzani.
“Mikutano hii haileti amani”
Kwa upande wa Moïse Katumbi, Olivier Kamitatu anaona mkutano huu kama “janja ambayo inatokana na mbinu ya kila mtu kujiokoa kwa kiongozi ambaye anataka kushikilia kiti chake kwa gharama yoyote.” Olivier Kamitatu badala yake anasisitiza haja ya mazungumzo kati ya Wakongo wote, msimamo ambao pia unashirikiwa na PPRD, chama cha Joseph Kabila ambacho kinasema suluhu la mzozo wa DRC ni kati ya Wakongo pekee.
“Majeshi yote ya kigeni lazima yaondoke katika nchi yetu na ni lazima tuanze mazungumzo. “Mikutano hii haileti amani,” anasema Ferdinand Kambere, mmoja wa makatibu wakuu wa chama cha rais wa zamani. Wote hawa wanarejelea mbinu ya viongozi wa kidini wa CENCO-ECC wanaoungwa mkono na vyama kadhaa vya upinzani.