DRC: Wakuu wa majeshi kutoka Uganda na Kongo wakutana ili kuratibu operesheni zao Ituri

Nchini DRC, mkuu wa majeshi ya nchi kavu wa FARDC, Jenerali Ndaywel, alikuwa Bunia siku ya Ijumaa kukutana na maafisa wakuu wa jeshi la Uganda. UPDF wameimarisha uwepo wao wiki hii katika mji huu, mji mkuu wa mkoa wa Ituri, kaskazini-mashariki mwa DRC. Lengo la mkutano huo lilikuwa kuratibu operesheni za pamoja kati ya nchi hizo mbili, chini ya makubaliano yaliyofikiwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita kuwasaka waasi wa ADF.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Tangu Jumatatu, wanajeshi wasiopungua 750 wa Uganda wamewasili na magari ya kivita. Wanajeshi hawa wako katika kambi ya FARDC, jeshi la Kongo, huko Rwampara nje kidogo ya Bunia.

Watapelekwa wapi na kwa kazi gani? Hili ndilo lengo zima la mikutano ya sasa. Mikutano ambayo anabainisha mratibu wa mashirika ya kiraia katika mko wa Ituri, Dieudonné Lossa: “Hii ni thibitisho kwamba kuwasili kwa askari wa Uganda sio mpango wa upande mmoja kwa upande wao … lakini ni jambo ambalo lilifikiwa na pande mbili yaani na serikali ya DRC. “

Kuingia kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Uganda kumesababisha wasiwasi …

Makubaliano hayo yaliyohitimishwa mwaka 2021 kati ya Kinshasa na Kampala yanatoa oparesheni ya pamoja dhidi ya waasi wa ADF, kama sehemu ya Operesheni Shujaa. Lakini vyanzo vya jeshi la Uganda vimeibua uwezekano kwamba vikosi hivi pia vitaendesha operesheni dhidi ya makundi ya waasi wenye silaha wa Kongo… wakati mzozo kati ya wanamgambo wa CODECO na Zaire hivi karibuni umeshika kasi…

Wiki iliyopita, mkuu wa majeshi wa Uganda pia alitishia, katika ujumbe uliotumwa kwenye mtandao wa kijamii, kuanzisha mashambulizi dhidi ya makundi yenye silaha ya Wakongo yanayoendesha harakati zao huko Bunia.

Hali ambayo inafanya raia kuwa na wasiwasi mkubwa kwa uwezekano wa kutokea Vita vya Pili vya Kongo, wakati Rwanda na Uganda zilipigana nchini DRC kupitia makundi hasimu yenye silaha.