
Wiki mbili baada ya kuingia Goma, wapiganaji wa M23 na wanajeshi wa Rwanda wanaowaunga mkono wanatafuta kuulinda mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, hasa katika viunga vya mji huo. Lakini katika jiji hilo, hali inaendelea kuwa mbaya kufuatia visa vingi vya wizi na uporaji, hali ambayo raia wanaona kuwa huenda ikawa mbaya zaidi katika siku zijazo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Raia wana hofu inapofika usiku, hasa kuporwa mali zao, kutokuwa na uhakika na ongezeko la silaha zilizotelekezwa mjini: hizi ndizo sababu kuu za wasiwasi kwa mkazi huyu wa Goma. “Inasemekana kuna majambazi wengi wenye silaha kwa sababu ya wingi wa silaha ambazo zimeachwa na mamluki hapa na pale. Kila usiku kuna milio ya risasi. Pia kuna mashambulizi ya kuvizia. Ni jambo lisiloeleweka… Hatujui kwa hakika kinachoendelea Goma kwa sasa,” anasema.
Kwa upande wake, M23 inabaini kwamba marufuku yote yameondolewa, ikiwa ni pamoja na marufuku yaliyokuwa yamewekewa kwa wanaoendesha pikipiki nyakati za usiku. Kundi hili lenye silaha pia limeanzisha kikosi cha kuingilia kati, anaeleza mfanyabiashara huyu: “Tatizo kubwa huko Goma ni ukosefu wa usalama. Visa vy uporaji na uvamizi wa nyumba usiku vmeanza. M23 imetoa nambari yake simu kwa kikosi chake cha kuingilia kati kwa watu wanaoshukiwa kuwa majambazi wenye silaha. “Ni kitu kipya na inatia moyo kidogo,” anakiri.
“Kwa kweli tunateseka sana, hakuna kinachoendelea hapa. “
Lakini kwa wakazi wengine wa mji mkuu wa Kivu Kaskazini, uwepo wa wapiganaji wa M23 huleta tu matatizo, yanayochochewa na mgogoro wa kiuchumi na chakula. “Mambo mabaya kila mara hutokea usiku. Watu wanauawa majumbani mwao. Tunajaribu kuona jinsi gani tunaweza kuzoea lakini, kwa bahati mbaya, tunateseka sana, hakuna kinachoendelea hapa,” anasema mmoja wao.
Wakiwa wametengwa, wakazi wa Goma, ambao wanaishi kwa kutarajia kufunguliwa tena kwa uwanja wa ndege wa kimataifa, pia wanatumai kufunguliwa tena kwa benki kwa sababu ukosefu wa pesa unazidisha hisia ya jumla ya ukosefu wa usalama katika jiji hilo.