DRC: Waasi wa M23 waudhbiti mji wa Bukavu, Kivu Kusini

Mji wa Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, unadhbitiwa na waasi wa M23 tang siku ya Ijumaa, Februari 14, wakiungwa mkono na jeshi la Rwanda.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo vilivyonukuliwa na Radio OKAPI, waasi wa M23 waliingia bila upinzani wowote huku raia wa kishuhudia.

Vyanzo hivyo vinaripoti kwamba muda mfupi kabla ya kuwasili kwa waasi hao katikamji wa Bukavu, askari wa jeshi la Kongo walikuwa tayari wameondoa ngome zao.

Hofu na kutokuwa na uhakika ulitanda kwa wakazi wa jiji walipoona kuondoka kusikotarajiwa kwa vikosi vya ulinzi na usalama.

Baada ya kutofahamishwa chochote, uvumi ulitanda pande zote.

Kwa baadhi ya wakazi wa mji huo, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini tayari umezingirwa na waasi hao wanaounga mkono Rwanda. Kwa hivyo wengine walibaini kwamba huenda ni mbinu za kimkakati za jeshi la DRC, FARDC, kutaka kukabiliana vilivyo na waasi hao.

vyanzo vingine kunlinagana na Radio OKAPI vimeripoti kuwa wanajeshi watiifu kwa serikali waliondoka katika jiji hilo kwa kuitikia wito wa mashirika ya kiraia kuwataka kuepuka umwagaji damu, kama ilivyotokea huko Goma.

Milio ya risasi ya hapa na pale iliyosikika jioni iliongeza hofu na kutengeneza imani moja kwamba waasi wameingia katika mji wa  Bukavu.

Baadaye kidogo, matukio ya uporaji yaliripotiwa katika baadhi ya maeneo ya jiji la Bukavu, kulingana na vyanzo vilivyovyonukuliwa na Radio OKAPI.

Ni katika hali hii ya hofu na kutokuwa na uhakika ambayo imewakuta wakazi wa Bukavu kwa usiku wa kuamkia leo.