DRC: Waasi wa M23 waripotiwa kushambulia ngome za wanajeshi wa FARDC

Mapigano mapya yameripotiwa mashariki ya DRC baada ya kipindi cha siku mbili za utulivu, waasi wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda wakiripotiwa kushambulia maeneo ya wanajeshi wa serikali huko Kivu Kusini.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Makabiliano hayo mapya yameripotiwa na vyanzo vya kiusalama kwenye eneo hilo. Jumamosi iliopita, wakuu wa nchi za SADC na wale wa EAC katika kikao cha pamoja, walitoa wito wa  kusitishwa mara moja kwa mapigano kwa kipindi cha siku tano.

Kuna hofu kwamba mapigano hayo ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu, wengine wakipoteza makazi yao yanaweza kusambaa hadi katika mataifa ya Ukanda.

Maelfu ya watu wamekimbilia katika kambi za wakimbizi wakitoroka mapigano kati ya waasi wa M23 na jeshi la serikali.
Maelfu ya watu wamekimbilia katika kambi za wakimbizi wakitoroka mapigano kati ya waasi wa M23 na jeshi la serikali. REUTERS – Arlette Bashizi

Waasi wa M23 katika siku za hivi karibuni wameripotiwa kuchukua udhibiti wa maeneo mbalimbali katika eneo la utajiri wa madini mashariki ya DRC.

Kundi la M23 lilianzisha uasi tena dhidi ya serikali ya DRC mwaka wa 2021.

Makabiliano hayo yameripotiwa siku ya Jumanne katika eneo la Ihusi, karibia kilomita 70 sawa na maili 43 kutoka katika Mji wa Bukavu na kilomita 40 kutoka kwenye uwanja wa ndege kulingana vyanzo vya kiusalama.

Mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa serikali ya DRC yamesababisha vifo vya maelfu ya watu katika Mji wa Goma.
Mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa serikali ya DRC yamesababisha vifo vya maelfu ya watu katika Mji wa Goma. AFP – ALEXIS HUGUET

Wanajeshi wa DRC wameripotiwa kuelekea katika Mji wa Kavumu, ambako uwanja wa ndege unapatikana ambapo kuna kambi ya jeshi ya eneo hilo kulingana na vyanzo vya kiusalama.

Raia wa Bukavu wamekuwa na hofu ya kushambuliwa na waasi wa M23 ambao wamekuwa wakidaiwa kuwa na njama ya kuingia kwenye mji huo.