Waasi wa M23 wanaosidiwa na Serikali ya Rwanda, jana jioni wametangaza kuwa hawatashiriki mazungumzo ya amani kati yake na Serikali ya Kinshasa yaliyokuwa yaanze hivi leo mjini Luanda Angola, saachache baada ya umoja wa Ulaya kutangaza vikwazo dhidi ya viongozi waandamizi wa kundi hilo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Miongoni mwa waliowekewa vikwazo ni pamoja na kiongozi wa kundi hilo, Betrand Bisimwa.
Uamuzi huu wa kushtukiza uliochukuliwa na M23, umekuja saa chache tangu kundi hilo lithibitishe kuwa litatuma wawakilishi Wake mjini Luanda, aumuzi ambao unatafsiriwa kuwa hauna nia njema.
Vikwazo vilivyotangazwa pia vinahusu makamanda wa juu wa jeshi la Rwanda, ambao umoja wa Ulaya umedai katika taarifa yake kuwa, kwa makusudi wanakwamisha juhudi za kupatikana kwa amani ya kudumu kwenue êneo la mashariki mwa nchi hiyo.
Kufuatia tangazo hili la M23, msemaji wa rais Felix Tshisekedi, Tina Salama, amesema serikali yao imetuma ujumbe Wake mjini Luanda kuonesha utayari wa kutaka suluhu na waasi hao ambao wanashikilia mji wa Goma na Bukavu.

Kwenye taarifa yake, uongozi wa M23 umesema uamuzi iliyouchukua umetokana na kampeni chafu za Kinshasa dhidi ya kundi hilo na kwamba hatua ya viongozi Wake kuwekewa vikwazo, haitoi mazingira sawia ya wao kushiriki mazungumzo.
Ikiwa mazungumzo haya hayatafanyika hivi leo, itakuwa pigo jingine kwa raia wa Congo ambao ndio wamekuwa wahanga wa machafuko yanayoendelea mashariki mwa nchi hiyo, M23 na Rwanda zikipewa shinikizo na jumuiya ya kimataifa kusitisha vita nchini DRC.