DRC: Vuguvugu la AFC/M23 latangaza kujiondoa Walikale-Centre

Wapiganaji wa vuguvugu la AFC/M23 wametangaza leo Jumamosi, Machi 22, kwamba watajiondoa kutoka Walikale-Centre, katika mkoa wa Kivu Kaskazini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),mji waliouteka siku ya Jumatano, Machi 19.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Matangazo ya kibiashara

Wanasema wanataka “kuweka mazingira mazuri, yanayofaa kwa mazungumzo,” kulingana na usitishaji mapigano uliotangazwa mwishoni mwa mwezi Februari. Lakini, kulingana na taarifa zilizokusanywa na RFI kutoka vyanzo vya ndani, wapiganaji hao bado wanaonekana katika angalau wilaya nne kati ya sita za jiji hilo.

Saa 8 mchana kwa saa za Afrika ya Kati, bado walikuwa katika maeneo hayo. Mashambulizi mapya ya anga yaliyofanywa na jeshi la Kongo yalilenga uwanja wa ndege wa Kigoma mapema asubuhi. Hali bado ni ya wasiwasi katika eneo hili la kimkakati mashariki mwa nchi, karibu kilomita 400 kutoka Kisangani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *