DRC: Viongozi wa makanisa washinikiza kuwepo kwa mazungumzo ya amani kati ya serikali na waasi

Viongozi wa kidini wa Kongo wanalenga kuandaa mazungumzo ya amani ambayo yataleta serikali ya Rais Felix Tshisekedi, waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda na viongozi wa upinzani walio uhamishoni kwenye meza moja, maafisa wawili wamesema siku ya Jumatano.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Juhudi hizo zingehitaji kumfanya Tshisekedi aachane na msimamo wake wa kukataa kuketi kenye meza moja na waasi, ambao anawataja kuwa magaidi. Lakini wakati M23 wakiendelea kusonga mbele baada ya kuteka miji miwili mikubwa mashariki mwa Kongo, waliohusika katika juhudi hizo wanasema wana matumaini.

M23 wanataka kupindua Felix Tshisekedi

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na serikali ya Rwanda, ambao wanaidhibithi miji ya Goma Bukavu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamesema wanataka kuendelea kupigana na kuipindua serikali ya Kinshasa.

Waasi walisema hayo wakati rais wa DRC Felix Tshisekedi alitoa wito wa jeshi kuimarishwa, na kuungwa mkono ili kukabiliana na waasi hao, huku Waziri wake wa ulinzi akifutilia mbali uwezekano wa kufanyika mazungumzo.

Waziri wa ulinzi wa DRC Guy Kabombo Muadiamvita, siku zilizopita alisema ameelekeza kwamba mipango yoyote ya mazungumzo na waasi wa M23 ifutiliwe mbali mara moja.

Katika ujumbe wa video, Muadiamvita alisema kwamba watapigana kabisa na kama watashindwa, watafia ndani ya Congo.

Waasi wa M23 wameonyesha lengo la kutaka kuongoza mashariki mwa DRC na kusema wapo tayari kwa mazungumzo na serikali ya Tshisekedi.

Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo Rwanda ni mwanachama pia imependekeza mazungumzo.