DRC: Viongozi wa kidini kutoka Cenco na ECC wakutana na upinzani waishio Ulaya

Mashariki mwa DRC, M23 na wanajeshi wa Rwanda sasa wanadhibiti mji wa Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini. Hatua iliyoshtumiwa na balozi kadhaa wa nchi za Magharibi. Wakati huo huo, viongozi wa kidini kutoka Kanisa Kikatoliki na Kanisa la Kiprotestanti wanaendelea na kazi yao waliojitolea ya mashauriano kama sehemu ya kile walichokiita “mkataba wa kijamii wa amani.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Kinshasa, Paulina Zidi

” Baada ya kukutana na Rais wa Kongo Félix Tshisekedi, viongozi wa AFC/M23 mjini Goma na Rais wa Rwanda Paul Kagame, sasa wako Ulaya.

Wajumbe wa Baraza la Kitaifa la Maaskofu wa Kongo (CENCO) na Kanisa la Kristo nchini Kongo (ECC) walikuwa mjini Brussels mwisoni mwa juma hili lililopîta kukutana na viongozi kadhaa wa upinzani wa kisiasa wa Kongo. Siku ya Jumapili, Februari 16, walizungumza na Moïse Katumbi na washirika wake.

Kama kawaida, wanadini waliwasilisha misheni yao, wakielezea mapatano yao ya kijamii, lakini zaidi ya yote walisikiliza. “Wanakusanya maoni ya wanasiasa na wadau mbalimbali kutoka DRC ili kuwasilisha ripoti kwa rais,” ameeleza mmoja wa washiriki wa mazungumzo hayo.

“Hakuna njia nyingine inayowezekana”

Upande wa Moïse Katumbi umehakikisha kwamba wanaunga mkono mbinu hii: “hakuna njia nyingine zinazowezekana”, wanabaini katika kambi ya mpinzani maarufu. “Wakongo wote lazima waketi kwenye meza moja ili kuzungumza wao kwa wao,” amesema Salomon Kalonga, seneta kutoka chama cha Ensemble pour la République.

Jumamosi 15, viongozi hao wa kidini walikutana na mbunge wa zamani Claudel Lubaya, lakini pia Jean-Claude Mvuemba na Franck Diongo, ambao walipata hadhi ya ukimbizi wa kisiasa nchini Ubelgiji. Na haswa na kambi ya Joseph Kabila, FCC, inayowakilishwa na Raymond Tshibanda, Nehémie Mwilamya na Joseph Makila.

Hatimaye, CENCO-ECC pia ilikutana na mwakilishi wa Umoja wa Ulaya kwa Maziwa Makuu.